Tuesday, 11 April 2017

Matumizi ya Simbomilia (Barcordes) katika bidhaa ni jambo lisilokwepeka Kuelekea Nchi ya Viwanda Tanzania

Matumizi ya Simbomilia (Barcordes) au alama za utambuzi wa bidhaa katika masoko ni jambo lisilokwepeka kwa sasa ambapo Tanzania inaelelekea kweye nchi ya uchumi wa kati na viwada. 

Haya yameelezwa na Mkurugezi wa Taasisi ya Global Standard one (GS1) Tanzania Bi. Fatma Kange Salehe wakati wa kutia saini ya makubaliano na Halmashauri nane za Mkoa wa Kigoma.

Mkataba wa Makubaliano na Taasisi ya GS1 Tanzania unalenga kuwapa mafunzo na kuwajengea uwezo wajasiriamali katika Halmashauri ili waweze kutambua umuhimu wa kuwa na alama za utambuzi wa bidhaa katika masoko wanazozizalisha.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuzijumuisha Taasisi mbalimbali zitakazoshiriki katika utoaji wa mafuzo hayo kwa wajasiriamali kama vile Wakala la Vipimo, Mamlaka ya Mapato Tazania, Shirika la Viwago Tanzania, BRELLA, SIDO, TANTRADE.

Matarajio baada ya mafunzo haya ni, kuongezeka kwa mapato ndani ya Halmashauri, bidhaa nyingi kuwa katika soko rasmi kitaifa na kimataifa, kuongeza mnyororo wa thamani ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali, kuongezeka kwa wajasiliamali katika Halmashauri na, kuwanyanyua kiuchumi wajasiliamali wadogo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (mst) ambaye alishuhudia utiwaji wa makubaliano hayo kati ya GS1 Tanzania na Halmashauri za Mkoa wa Kigoma alisema kuwa lengo la Serikali ya Mkoa wa Kigoma ni kuhakikisha kwamba fursa zote za kilimo, uvuvi na madini zinafanyiwa kazi kisasa zaidi ili wananchi waweze kumiliki Uchumi. “ili wananchi wetu waweze kunufaika na kilimo, vuvi, madini  lazima kuwepo na mbinu sahihi za kuongeza thamani kwenye bidhaa zao wanazozalisha na zikubalike katika masoko ya ndani nje” alisisitiza.

“Ninaamini makubaliano haya yatakuwa na matokeo chanya ambayo yatawezesha bidhaa nyingi za Tanzania hususani wananchi wa Kigoma kuingia katika Masoko ya ndani na nje ya nchi hivyo kuinua pato la mtu mmoja mmoja na hatimae taifa zima” aliongeza Maganga.

Aidha, amewaasa watanzania kuanza kutumia Simbomilia (barcordes) za Tanzania badala ya kutumia za nje ya nchi. Alisisitiza kuwa kutumia simbomilia za Tanzania kutapunguza matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kulipia uduma hiyo, pia itasaidia kutoa takwimu rasmi za wazalishaji wa Kitanzania, kwani unapotumia simbomilia za nje ya nchi bidhaa huonekana imetoka nchi nyingine na siyo Tanzania hata kama imezalishwa hapa nchini.

Kutokana na umuhimu wa jambo hili Maganga amewaagiza Wakurugenzi kuanza mafunzo haya kwa wajasiliamali ndani ya Miezi miwii tangu kutiwa saini ya Makubaliano na Taasisi ya GS1 Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (katikati), Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Charles Pallangyo (kulia) na Mkurugenzi wa GS1 Tanzania Bi Fatma Kange Salehe wakishuhudia utiaji wa saini kati ya Tasisi hiyo na Halmashauri ya Kakonko.

Thursday, 26 January 2017

Mkoa wa Kigoma Wateketeza zana Haramu za Uvuvi

Jumla ya zana haramu za uvuvi 343 zenye thamani zaidi ya Shilingi za kitanzania 480,000,000 zimeteketezwa moto Mkoani Kigoma, ikiwa ni hatua ya Serikali ya Mkoa kupambana na Uvuvi usioendelevu.

Zana hizo zilikamatwa na vikosi vya doria ziwani kwa vipindi tofautitofauti katika ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma.

Uvuvi wa Kutumia zana haramu katika Ziwa Tanganyika umekuwa tishio katika Mwambao wa Ziwa hilo ukiashiria kupoteza kabisa samaki na dagaa ambao ni kitoweo muhimu kwa wakazi wanaolizunguka Ziwa Tanganyika na kwingineko.

Akiongea wakati wa Zoezi la Uchomaji wa Zana hizo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Charles Pallangyo alisema zoezi hili ni endelevu kwani Mkoa wa Kigoma hautamvumilia Mtu yeyote kutumia zana za Uvuvi zisizo na tija katika kuendeleza Uvuvi endelevu.

Pallangyo amewataka wavuvi kufuata taratibu na sheria za matumizi ya zana za Uvuvi ili kulinda Rasilimali za Ziwa Tanganyika kuwa endelevu kwa faida ya Vizazi vijavyo.

Naye Afisa Uvuvi wa Mkoa wa Kigoma Bi. Ritta Mlingi amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuwa hakuna samaki anayevuliwa kwa sumu kama ilivyokuwa inavumishwa na watu.

Aliongeza kuwa zana za uvuvi zinapokamata samaki hupandishwa mtumbwini saa hiyohiyo isipokuwa zana za “makila” ambazo huachwa hadi asubuhi ndipo huteguliwa na kupandishwa kwenye chombo.

Hivyo samaki wanaokamatwa mapema na “makila” hufa mapema kutokana na kukabwa sehemu za mapezi “Gills” , kasi yake kwa kuharibika huwa ni kubwa uizingatia wavuvu wengi hawana Barafu kwaajili ya kutunzia samaki ndani ya ziwa.

“Nawaomba wananchi wasiwe na wasiwasi kwani samaki hawanasumu isipokuwa kukosekana nyenzo bora za utunzaji pindi wanapovuliwa, hata hivyo mwanchi yeyote atakayekuwa na ushahidi wa samaki mwenye sumu anakaribishhwa kuleta usahidi huo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa” aliongeza Mlingi.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (Mst.) Mhe. Emannuel Maganga akiweka moto katika Nyavu na zana haramu za kuvulia zilizokamatwa katika Mkoa wa Kigoma

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Charles Pallangyo akiungana na Wadau mbalimbali katika zoezi la uteketezaji wa zana haramu za kuvulia samaki na dagaa Mkoani KigomaZaidi ya silaha haramu 5600 zimeteketezwa moto Mkoani Kigoma


Zaidi ya silaha haramu 5600 zimeteketezwa moto Mkoani Kigoma ikiwa ni moja ya hatua za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa silaha haramu nchini.

Akiongoza zoezi la uteketezaji wa silaha hizo Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba alisema “tatizo la uzagaaji wa silaha ni la kidunia, kwa kiwango kikubwa uzagaaji wa silaha hovyo umeathiri maendeleo kiuchumi, kisiasa na Kijamii”

Aidha ameongeza kuwa tangu Januari 2017, amefuta ukimbizi wa Makundi kama ilivyokuwa awali na utaratibu utakuwa kila Mkimbizi ataingia nchini baada ya kuhojiwa na kujadiliwa na Kamati husika.

Alitoa rai kwa Watazania wote wanaomiliki Silaha kinyume na taratibu za nchi kuzisajili au kuzisalimisa silaha hizo, na mwisho wa zoezi hilo itakuwa tarehe 30 Juni, 2017, baada ya hapo hatua kali za watakaobainika zitachukuliwa.

Silaha zilizoteketezwa zilikamatwa kutoka katika Mikoa ya Mara, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Katavi, Rukwa, Kagera na Kigoma.

Hata hivyo Mkoa wa Kigoma umetajwa kuongoza kwa uzagaaji wa Silaha haramu kwa asilimia zaidi ya 40%  na matukio yanayohusisha silaha kwa 20 % ukiligaishwa na Mikoa Mingine.

Akizungumza katika zoezi la Uteketezaji wa Silaha hizo Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani Msanzya alisema Mkoa wa Kigoma unaogoza kutokana na kupakana na nchi zenye machafuko ya Kisiasa, kupokea wakimbizi wengi  ambao huingia kwa makundi bila kupekuliwa, baadhi yawakimbizi wasio waaminifu hutumia mwanya wa ukimbizi vibaya kwa kufanya matendo mengi ya kihalifu.

Hadi sasa wakimbizi waliopo Mkoani Kigoma ni zaidi ya 27,000 ambao ni chimbuko la uzagaaji wa silaha haramu Mkoani Kigoma. Imeelezwa kuwa katika Mkoa wa Kigoma kwa siku hupokea wakimbizi 400 hadi 500 wakitokea Nchi jirani za Burundi na Congo.

Hata hivyo taarifa  zinasema wengi wao sasa hawakimbi kwa hofu ya machafuko ya kisiasa bali wanakimbia njaa na ugumu wa maisha nchini mwao.

Naye Naibu Kamishna wa Polisi Sekretarieti ya Umoja wa Kikanda wa Kushughuliikia uzagaaji wa silaha Bw. Theonest Mshindashaka alisema Jumla ya Silaha zilizokwisha kuteketezwa kati ya 2014 hadi 2017 ni zaidi ya 17,000.

Uteketezaji wa silaha haramu umefadhiliwa na Serikali ya Marekani Kitengo cha Kupambana na Uzagaaji wa Silaha.

Silaha mbalimba za moto zipatazo 5608 zikiwa zimeandaliwa tayari kwa Kuteketezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma


Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (MB) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali (Mst.) Emannuel Maganga muda mchache kabla ya kuteketeza Silaha haramu.


Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (MB) akiwasha moto Silaha haramu kupitia Mfumo maalumu wa ulipuajiHabari zote na

G.D. Ng'honoli

  Afisa Habari na Mawasiliano wa Sekretarieti ya Mkoa wa

 Kigoma

Wednesday, 14 December 2016

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA NA MANISPAA YA KIGOMA UJIJIMkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akisikiliza kero mbalimbali katika Kijiji cha Nkungwe Wilayani Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (mwenye koti) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Samson Anga (kulia) wakiwa katika kazi ya kukagua Miundombinu katika kijiji cha Bitale iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Meneja wa SIDO Mkoa wa Kigoma Bw. George Ntahamba akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga wa namna SIDO inavyowasaidia wajasiriamali  Mkoani Kigoma. 


Sehemu ya eneo la SIDO lililotengwa maalum kwa Shughuli za kuchakatia mazao ya mchikichi.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akikagua taarifa ya mapato na matumizi katika kijiji cha Mayange baada ya kuelezwa kuwa uongozi wa kijiji hautoi taarifa za mapato na matumizi ya kijiji hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (mwenye shati la kitenge) akikagua Miundombinu ya stendi ya Mabasi ya Mkoa wa Kigoma iliyopo eneo la Masanga katika Manispa ya Kigoma Ujiji.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akitoa maelekezo ya uboreshaji Miundombinu katika Soko la Mwanga Sokoni lililopo eneo la Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Vichanja vya Kisasa vitakavyotumika kuanikia dagaa katika Mwalo wa Kibirizi ufukweni mwa Ziwa Tanganyika, vichanja hivyo vimejengwa kwa msada kutoka Shirika la Maendeleo la Ubelgiji.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Mwanga Manispaa ya Kigoma Ujiji Bw. Raymond Ndhabhiyegetse akitoa maelezo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga kuhusu kero mbalimbali zinazolikabili soko hili.


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akisikiliza kero kutoka kwa wafanyabiashara eneo la Mwalo wa Kibirizi uliopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.


Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Moses Msuluzya akitoa ufufanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga wakati wa kukagua na kusikiliza kero katika Soko la Mwanga Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akikagua utunzaji wa vyanzo vya maji katika kijiji cha Kagongo Katika Halmshauri ya Wilaya ya Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga wakikagua ujuenzi unaoendelea katika daraja dogo katika kijiji cha Bitale iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akitembelea maeneo mbalimbali ndani ya Soko la Mwanga Sokoni lililopo eneo la Manispaa ya Kigoma Ujiji.


Habari zote na

G.D. Ng'honoli


  Afisa Habari na Mawasiliano wa Sekretarieti ya Mkoa wa


 Kigoma

Saturday, 3 December 2016

Watumishi Mkoani Kigoma Wahimizwa Kufanya Mazoezi ya Mwili kama sehemu ya Kuboresha Afya.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Generali (Mst.) Emannuel Maganga leo ameongoza na kushiriki mazoezi ya mbio kwa umbali wa kilomita 12 zilizolenga kuhamasisha watu wapende kufanya mazoezi ya mwili ili kuimarisha Afya zao.

Mbio hizo zilizoandaliwa na Kigoma Jogging Club zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, watumishi kutoka Sekretarieti ya Mkoa  na Taasisi mbalimbali za Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Katika kuhitimisha mbio hizo Brigedia Generali (Mst.) Maganga amewashukuru Uongozi wa Kigoma Jogging Club kwa kuanzisha mazoezi hayo ambayo ni muhim kwa afya “ nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza ninyi mliofikiri kuanzisha kitu kama hiki kwani leo tulivyokimbia pamoja tumepata faida nyingi, ukiachiliambali kujenga afya tumefahamiana na kujenga umoja, hata hivyo baadhi yetu hufanya mazoezi haya kwa ratiba zao lakini tunapokuwa pamoja hivi tunatiana moyo zaidi kuliko mtu akifanya mazoezi peke yake anaweza kujisikia uvivu na kuacha”


Aidha amewaasa watumishi wote na wananchi kupenda kufanya mazoezi kama njia ya kuondokana na maradhi mbalimali mathalani shinikizo la damu. “Ninawaomba msiishie leo tu, mazoezi haya yawe endelevu kwa ajili ya faida ya afya zetu” 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Generali (Mst.) Emannuel Maganga akiwa na Wakuu wa Taasisi, Idara mbalimbali wakati wa kukimbia mbio za uhamasishaji Mazoezi

Mkuu wa Mkoa wa Kgoma (mwenye fulana nyekundu) Mhe. Brigedia Generali (Mst. ) Emanuel Maganga akiongoza mazoezi ya kukimbia (kushoto kwake) ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Samson Anga (kulia kwake) ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma Bw. Daniel Machunda.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Generali (Mst.) Emannuel Maganga (Mwenye fulana ya drafti) pamoja na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma Bw. Daniel Machunda. (mwenye fulana ya bluu) wakihitimisha zoezi la mbio za kuhamasisha mazoezi  kwa kuimba wimbo wa Mchakamchaka Katika Uwanja wa Michezo wa Lake Tanganyika.

Watumishi kutoka sekta mbalimbali katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wakishiriki mbio za uhamasishaji wa Mazoezi kama sehemu ya kuboresha Afya zao.

Baadhi ya watumishi wa Taasisi mbalimbali za Serikali walioshiriki katika mbio za uhamasishaji mazoezi zilizofanyika Siku ya Jumamosi tarehe 03 Disemba, 2016 Katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.Picha zote na

G.D. Ng'honoli
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma


Tuesday, 29 November 2016

Zaidi ya Wanafunzi 17,854 kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2017 Mkoani Kigoma

Jumla ya wanafunzi 17,854 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2017, kati yao wavulana ni 9931 na wasichana 7923 Kati ya wanafunzi hao wanafunzi watakaosoma shule za Bweni ndani na nje ya Mkoa wa Kigoma ni 92 na sekondari za kutwa ni 17,762.

Watahiniwa 19,062 kati yao wavulana 10,738 na wasichana 8,324 ambao ni sawa na asilimia 70.79 walifaulu Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2016  uliofanyika tarehe 07 – 08 Septemba, 2016 katika Mkoa wa Kigoma  kwa kupata alama kati ya 100 na 250. Ufaulu huo ni ongezeko la silimia 16.75 ukilinganisha na ufaulu wa asilimia 54.04 kwa watahiniwa wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2015. 

Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Mitihani wa Mkoa katika kikao cha kutangaza Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kuendeleza na kidato cha kwanza Januari 2017, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Moses Msuluzya alisema Ufaulu huo umeufanya Mkoa wa Kigoma kushika nafasi ya 11 kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Msuluzya aliongeza kuwa Ufaulu huo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na walimu kujituma, usimamizi madhubuti wa Halmashauri na Mkoa.  Aidha, utoaji wa Elimu bila malipo kuanzia Elimu ya Msingi hadi kidato cha Nne pia umechangia ongezeko la ufaulu katika Mtihani huu.

Aidha Wanafunzi 1208 wakiwemo wavulana 807 na wasichana 401 wenye alama za ufaulu kuanzia 100 wamekosa nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2017 kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa. 

Hata hivo wanafunzi hao 1208 watachaguliwa kuingia kidato cha kwanza ifikapo Februari, 2017 baada ya Halmashauri kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vya kuweza kuchukua wanafunzi hao waliobaki.  Halmashauri ambazo wanafunzi waliofaulu lakini wameshindwa kupata nafasi kuingia kidato cha kwanza ni Kasulu Mji wanafunzi 568 na Uvinza wanafunzi 568. 

Aidha Msuluzya alitoa wito kwa wazazi/walezi na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza kuanza masaomo maramoja ifikapo Januari, 2017.  Hatua za kisheria zichukuliwe kwa yeyote atakayekwamisha au kuzuia mwanafunzi aliyechaguliwa kuendeleza na masomo ya sekondari.

Kuhusu suala la madawati Msuluzya amewakumbusha kuwa wahakikishe kila mwanafunzi aliyechaguliwa na anayeendelea na masomo anakaa kwenye dawati kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha, zoezi la utengenezaji madawati, viti na meza litakuwa endelevu katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma na hakuna ruksa ya kuchangisha mchango katika shule za Msingi na Sekondari.


Mkoa wa Kigoma ulikuwa na watahiniwa 27,111 kati yao wavulana 13,574 na wasichana 13,537 waliokuwa wamesajiriwa kufanya mtihani.  Watahiniwa waliofanya mtihani huo Septemba, 2016 ni 26,928 kati yao wavulana ni 13,468 na wasichana 13,460.  Watahiniwa 183 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ugonjwa na vifo.

Thursday, 19 June 2014