Friday 24 November 2023

Wanane wafariki kwa Ajali Wilayani Kibondo

Watu wanne wamefariki Dunia na wengine Sita kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya gari ndogo aina ya Toyota Succeed yenye Namba T890 DYZ iliyokuwa ikisafirisha abiria katika wilaya za Kibondo na Kakonko kugongana na gari aina ya Faw yenye namba T833 DUA mali ya Kampuni ya CHICO katika kijiji cha Kamkugwa wilayani Kibondo mkoani Kigoma. 


Akitoa Taarifa kwa vyombo vya Habari, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye  amewataja waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea Desemba 23, 2023 kuwa ni Dereva na mmiliki  wa gari ndogo Hamis Chaurembo(27), waliokuwa abiria Bernadina Reuben(22), Maduha Asukile  Ntinganiza Bihezako(67) Vedastus Paul(28), Vladmir Vedastus (1) na marehemu wengine wawili majina yao bado hayajafahamika.


Andengenye amewataja majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni Flavianus Felician(28), Juma Said,(27), Daniel Samwel(33),  Silvanus Muhingwa(43), Sara Bundala (20) na Doris Mafumbo(22) ambapo watatu kati yao wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi huku wengine watatu wakiendelea na matibabu yao katika Hospitali ya wilaya Kibondo. 


Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa Rai kwa  kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri mkoani Kigoma kuendelea kuchukua tahadhari ikiwemo kuzingatia Alama za usalama barabarani pamoja na kuepuka mwendo kasi. 


Pia Andengenye ametumia fursa hiyo kuikumbusha jamii mkoani hapa kuchukua tahadhari mbalimbali za kiusalama hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

No comments:

Post a Comment