Wakala
wa Majengo Tanzania TBA wameonywa kuwa na tabia za ucheleweshaji wa kumaliza
miradi mbambali wanayopewa na Serikali jambo ambalo linakwamisha utoaji wa
huduma katika miradi hiyo kama ilivyokusudiwa.
Serikali
ilitoa fedha kwaajili ya ukarabati wa miundombinu kwa shule na vyuo vya zamani
ambazo majengo yake na miundombinu ilikuwa imeshaakaa, kwa Mkoa wa Kigoma shule
1 ikiwemo Shule ya Sekondari ya Kigoam iliweza kupatiwa shilingi milioni 900,
ambapo Mkandarasi Wakala wa Majengo Mkoani alipatiwa kazi hiyo.
Hata
hivyo kumekuwa na kasi ndogo pamoja na utendaji usio wa kurishisha katika
kufanya ukarabati wa miundombinu katika shule hiyo, kitendo ambacho kimefanya
kuchelewa kukamilishwa kwa huduma muhimu kama vile vyoo, mabafu na mabweni.
Hadi
kufikia muda wa wanafunzi kurudi kuanza muhula mwingine wa masomo mwaka 2018
bado wakala wa majengo Mkoani Kigoma walikuwa bado hawajakamilisha ukarabati wa
miundo mbinu ikilinganishwa na fedha mabayo tayari imekwishakutolea awamu ya
kwanza shilingi milioni 400.
Hali
hii inamtia hasira si Waziri wa Elimu peke yake bali hata Mkuu wa MKoa wa
Kigoma ambapo walipofanya ziara ya kukagua kazi zilizofanywa, ikaonekana ni mchezo
wa kuigiza.
Akizungumza
katika ziara ya kukagua ukarabati wa shule ya sekondari Kigoma Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alimwambia Meneja Wakala wa
Majengo Mkoani Kigoma kuacha ubabaishaji na kuendana na kasi ya serikali ya
awamu ya tano.
Inaonekana
meneja hujui kazi yako, haiwezekani tangu mwezi Agosti 2017 mpaka leo hii
hakuna kazi ya kuonekana uliyokwisha imaliza, wanafunzi wanasiku tatu wafungue
bado vyoo havieleweki, unacheza na maisha ya binadamu, hili halikubaliki katika
serikali ya awamu ya tano alisisitiza Prof. Ndalichako
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. Mstaafu Emmanuel Maganga ameshangazwa na
kitendo cha wakala wa Majengo Mkoani Kigoma cha kushindwa kumaliza ukarabati
wa Shule ya sekondari ya Kigoma pamoja
na kuwa Serikali imeshatoa fedha karibu nusu ya gharama kwaajili ya ukarabati
tangu Agosti, 2017.
Kufuatia
hatua hiyo amabayo inaashiria uzembe, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma aliamuru kuwekwa
mahabusu Meneja wa Wakala Mkoani Kigoma Bw. Mgalla Mashaka kwa uzembe wa
usimamizi na kushindwa kutoa maelezo sahihi ya nini kilichokwamisha
kutomalizika kwa ukarabati wa shule hiyo.
No comments:
Post a Comment