Friday 15 December 2023

MAAFISA UTUMISHI WASIWE KIKWAZO KWA WATENDAJI

 


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka wafanyakazi wa idara za utumishi mkoani humo kushughulikia changamoto za kiutumishi zinazowakabili wafanyakazi kwa wakati ili kuondoa manung'uniko yanayopunguza ari ya watendaji

Kauli ya Andengenye imekuja kufuatia baadhi ya watumishi wilayani Kakonko kulalamikia kutopandishwa madaraja kwa wakati na wengine wakiwa na madai ya mapunjo mishahara na posho za uhamisho kwa muda mrefu bila ya kuwa na majibu yanayojitosheleza

Watumishi hao wamesema licha ya kufuatilia changamoto hizo kwa muda mrefu katika mamlaka husika lakini hawajapata ufumbuzi na kumuomba mkuu wa mkoa huo aingilie kati kuwasaidia kupata haki zao



   ANASATZIA ATANASI- MUUGUZI NA RAHIM SWALEHE- AFISA MIFUGO

Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewaagiza viongozi wa wilaya mkoani humo kuwawezesha na kuwasimamia mafias utumishi ili wawe mstari wa mbele kufuatilia ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili watumishi



Andengenye amesisitiza kuwa ni jukumu la maafisa Utumishi kufuatilia stahiki za wafanyakazi badala ya watumishi kutumia muda mwingi kuto wahudumia wananchi na kuhangaika kutafuta haki zao katika mamlaka mbalimbali.

Andengenye ameanza leo ziara ya siku tisa kukagua maendeleo ya miradi ya maendeleo katika wilaya za Kakonko na Kibondo na kuzungumza na watumishi na wananchi katika maeneo atakayokagua miradi hiyo.



No comments:

Post a Comment