Tuesday 19 December 2023

UJENZI SHULE YA MSINGI MAHAHA KUWAONDOLEA ADHA WANAFUNZI KUTEMBEA KM 20

Ujenzi wa Shule ya Msingi Mahaha  umetajwa kuwaondolea adha ya kutembea zaidi ya Km. 20 wanafunzi kutoka Kitongoji cha Mahaha kilichopo kijiji cha Magalama Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma. Baadhi ya wakazi katika kitongoji hicho wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwasogezea huduma hiyojirani kwani itaimarisha Usalama wa watoto wao kwenda na kurejea kutoka shule.

"Watoto wengi walikuwa watoro, wengine waliacha shule na hata baadhi ya wazazi kuhofia kuwaandikisha watoto Elimu awali na Msingi kutokana watoto hao kutomudu kutembea umbali huo pamoja na kuhofia  usalama wao wakiwa njiani kwani kuna nyakati hurejea nyumbani usiku au hunyeshewa na mvua" ameeleza Theresia Kanwa.

Akitoa Taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Afisa Elimu Awali na Msingi Oliver Mgeni amesema Miundombinu imekamilika na kuanzia Januari 2024 itapokea wanafunzi  wa Elimu Awali na Msingi kuanzia Darasa la kwanza hadi la Saba.


Tunaishukuru serikali kupitia mradi wa BOOST kwa kutenga fedha kiasi cha Shilingi 361,500,000 ili kujenga Shule hii kwani watoto wote kutoka kitongoji cha Mahaha waliokuwa wakisoma katika kijiji cha Magalama watarejeshwa hapa ili wasome katika shule hii ya kisasa iliyojengwa jirani na makazi yao" amesema Oliver Mgeni kupitia taarifa hiyo


Baadhi ya wakazi katika kitongoji hicho wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwasogezea huduma hiyojirani kwani itaimarisha Usalama wa watoto wao kwenda na kurejea kutoka shule.

"Watoto wengi walikuwa watoro, wengine waliacha shule na hata baadhi ya wazazi kuhofia kuwaandikisha watoto Elimu awali na Msingi kutokana watoto hao kutomudu kutembea umbali huo pamoja na kuhofia  usalama wao wakiwa njiani kwani kuna nyakati hurejea nyumbani usiku au hunyeshewa na mvua" ameeleza Theresia Kanwa.





MSIWAANGAMIZE WATOTO WENU

 Mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye ametoa wito kwa wananchi wa jamii ya wafugaji na wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini kutumia fursa ya uwepo wa miundimbinu bora ya elimu inayojengwa na serikali kuwasomesha watoto wao

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza na wananchi wa kata ya Nyamtukuza wilayani Kakonko na kusema elimu ndio dira itakayomsaidia mtoto kuyamudu mazingira anayoishi na kuacha kuwasomesha watoto ni kuaangamiza mustakabali wao maisha yao katika siku za usoni. 

KAULI YA Andengenye imekuja kufuatia serikali kujenga shule ya sekondari katika kitongoji cha LUTENGA katika wilaya ya KAKONKO mahali ambapo wengi wanaoishi hapo ni wafugaji na wachimbaji wa madini waliohamia miaka ya hivi karibuni.

Wakazi wa Lutenga kata Nyamtukuza wilayani Kakonko wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kigoma mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari katika kitongoji hicho.
Mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondri katika kitongoji cha Lutenga

Wanafunzi wa maeneo hayo walikuwa wakisumbuka kutembea umbali wa zaid ya kilomita thelathini kufuata elimu ya sekondari katika kijiji cha Nyamtukuza na kusababisha wengine kukatiza masomo kwa kushindwa kumudu adha hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kakonko MHULI NDAKI akitoa taarifa ya ujenzi wa shule ya sekondari katika kitongoji cha Lutenga na kusema serikali imetoa jumala ya shilingi Bilioni moja na milioni mia mbili kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya, shule na soko katika kata ya nyamtukuza na utekelezaji wa miradi yote hiyo upo zaid ya asilimia tisini na kutarajiwa kukamilika mapema mwezi ujao

Kwa upande wao wananchi wa kata hiyo wameishukuru serikali kwa ujenzi wa miradi ya maendeleo katika eneo lao na kuwaondolea adha ya kusafiri kwenda wilaya Biharamulo mkoani Kagera kufuata huduma mbalimba za kijamii ilihali kiutawala wapo wilaya ya kakonko mkoani Kigoma

Sunday 17 December 2023

UKIHUJUMU MIUNDOMBINU YA UMMA HUMKOMOI KIONGOZI

Wanafunzi wa shule za msingi kutoka vitongoji vya NYAKASERO,  MURUGABA na MKUYUNI katika kijiji cha NYAMTUKUZA wilayani KAKONKO Mkoani KIGOMA wameondokana na adha ya kutembea umbali wa zaid ya kilomita kumi kwa miguu kufuata elimu katika shule ya msingi Nyamtukuza.

Kero hiyo imeondoka baada ya serikali kutoa Zaid ya shilingi milioni 360 kupitia mradi wa Boost kwajili ya ujenzi wa shule mpya ya mfano yenye viwango vya kimataifa ambayo tayari imekamilika kwa asilimia mia moja.

Shule hiyo yenye michoro, Bembeya na maeneo ya michezo kwaajili ya watoto wadogo inatajwa kuwa moja ya shule chache za msingi zenye viwango vya kimataifa zilizopo mkoani Kigoma na kutarajiwa kuanza kutumika januari mwakani.

Mkuu w mkoa wa kigoma Thobias Andengenye akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi wa kwanza wa kulinda miundoimbinu ya umma waliojengewa na serikali ili iweze kuwahudumia kwa muda mrefu

Andengeye akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Murugamba na Nyakasero na kusisitiza kuwa serikali haitawafumbia macho watu watakao bainika kuihujumu miundombinu ya serikali na kama wenyeji wa maeneo  hayo wakifumbia macho na kutotoa taarifa ya ubadhirifu au wizi wa aina yoyote katika miundombinu inayowahudumia itawasababishia watoto wao kukosa huduma muhimu karibu na maeo yao

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko MHULI NDAKI akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Kigoma kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya mfano na kusema licha ya mradi huo kutokuwa na gharama za ununuzi wa samani lakini ofisi yake imeshaweka utaratibu wa kuhakikisha shule hiyo inakuwa na samani za kisasa zenye hadhi sawa na majengo hayo

Friday 15 December 2023

MAAFISA UTUMISHI WASIWE KIKWAZO KWA WATENDAJI

 


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka wafanyakazi wa idara za utumishi mkoani humo kushughulikia changamoto za kiutumishi zinazowakabili wafanyakazi kwa wakati ili kuondoa manung'uniko yanayopunguza ari ya watendaji

Kauli ya Andengenye imekuja kufuatia baadhi ya watumishi wilayani Kakonko kulalamikia kutopandishwa madaraja kwa wakati na wengine wakiwa na madai ya mapunjo mishahara na posho za uhamisho kwa muda mrefu bila ya kuwa na majibu yanayojitosheleza

Watumishi hao wamesema licha ya kufuatilia changamoto hizo kwa muda mrefu katika mamlaka husika lakini hawajapata ufumbuzi na kumuomba mkuu wa mkoa huo aingilie kati kuwasaidia kupata haki zao



   ANASATZIA ATANASI- MUUGUZI NA RAHIM SWALEHE- AFISA MIFUGO

Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewaagiza viongozi wa wilaya mkoani humo kuwawezesha na kuwasimamia mafias utumishi ili wawe mstari wa mbele kufuatilia ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili watumishi



Andengenye amesisitiza kuwa ni jukumu la maafisa Utumishi kufuatilia stahiki za wafanyakazi badala ya watumishi kutumia muda mwingi kuto wahudumia wananchi na kuhangaika kutafuta haki zao katika mamlaka mbalimbali.

Andengenye ameanza leo ziara ya siku tisa kukagua maendeleo ya miradi ya maendeleo katika wilaya za Kakonko na Kibondo na kuzungumza na watumishi na wananchi katika maeneo atakayokagua miradi hiyo.



Wednesday 13 December 2023

TAKWIMU NI MUHIMU, MKUU WA MKOA WA KIGOMA THOBIAS ANDENGENYE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUSISITIZA UMUHIMU WA TAFITI MBILI ZINAZOENDELEA KUFANYIKA MKOANI HUMO.

 Serikali imewataka wananchi kuwapa ushirikiano watafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wanaozunguka katika maeneo mbalimbali nchini ili zipatikane tawimu sahihi zitakazoweza kutumika katika kufuatailia na kutathmini utekelezaji wa mipango na program za maendeleo katika ngazi ya taifa, kikanda na kimataifa.

Kauli hiyo ya serikali imekuja kufutia kuanza kwa tafiti mbili  katika sekta ya kilimo,  kiuchumi na kijamii katika mikoa yote ya TANZANIA Bara na ZANZIBAR zikilenga kubaini ufanisi wa program zilizopo na changamoto zinazowakabili wananchi katika sekta hizo



.Waafiti kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu wamesema tafiti hizo tayari zimeanza kufanyika kuanzia tarehe tano novema ikihusisha mikoa yote  ya tanzania bara na visiwani ambapo jumla ya maeneo 1352, maeneo 1234 yapo Tanzania bara na maeneo 118 ni kutoka Zanzibar  kwa kuzihusisha kaya 16224, 14808 kutoka Tanzania bara na 1416 kutoka Tanzania Zanziba

    SUMA TEBELA, MENEJA WA NBS MKOA WA KIGOMA AKIWA NA  ENDREW PUNJIRA, AFISA MASOKO WA NBS WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUELEZEA MAENDELEA TAFITI ZILIZO ANZA KUFANYIKA NOVEMBA TANO MWAKA HUU NA KUTARAJIWA KUDUMU KWA KIPINDI CHA MIEZI MIWILI KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI

Watafiti hao kutoka ofisi ya taifa takwimu wamesema tafiti hizo ni muhimu kwa manufaa ya umma ambapo tafiti za kiuchumi na kijamii zitahusisha majengo na shughuli zote za kiuchumi zilizopo ilihali tafiti za kilimo zitahusisha mashamba makubwa na madogo katika kilimo na ufugaji.

Saturday 9 December 2023

ANDENGENYE AHIMIZA VITA DHIDI YA UJINGA, MARADHI NA UMASIKINI ILI KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU

Posted On: December 9th, 2023

Jamii mkoani Kigoma imetakiwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi zake za kukabiliana na maadui Ujinga, Maradhi na Umasikini ili kuufanya Mkoa na Taifa kwa ujumla kuweza kuwa na Uchumi imara na kujitegemea.

Kauli  hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alipozungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kigoma, ambapo amesisitiza jamii kujenga tabia ya kufanya kazi kwa bidi ili kujiimarisha kiuchumi.

Amesema iwapo Jamii itafanikiwa kukabiliana na maadui hao watatu na kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa ufasaha, kujituma pamoja na kudumisha amani na utulivu, uchumi wa mwananchi mmoja mmoja utazidi kuimarika na kulifanya  taifa kusonga mbele.

‘‘Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu anaendelea kuendesha mapambano dhidi ya maadui hao kwa kuboresha miundombinu mbalimbali inayoleta ufanisi katika utoaji wa huduma za jamii pamoja na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi’’ amesema Andengenye.

Andengenye amesema mkoa wa Kigoma unajivunia mapinduzi makubwa ya Miundombinu yanayoendelea kufanyika ikiwemo ukarabati wa Uwanja wa Ndege, Ujenzi wa Barabara mbalimbali kwa kiwango cha Lami, mkoa kuunganishwa na Umeme wa Gridi ya Taifa, uboreshwaji mkubwa wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia, ujenzi wa vyuo vikuu pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Aidha katika kutekeleza shughuli mbalimbali zinazokwenda sambamba na maadhimisho hayo, Mkuu huyo wa Mkoa amegawa miche zaidi ya 2000 ya zao la chikichi kwa wakazi wa Kata ya Machinjioni kisha kuhitimisha maadhimisho hayo kwa kushiriki kufanya usafi katika soko la Nazareti katika  Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli amehimiza jamii wilayani humo kujenga Tabia ya kudumisha usafi ili kupunguza athari mbalimbali zinazoweza kusababishwa na maradhi na kupunguza nguvu kazi ya Taifa.

‘’Nashauri tabia hii ya kufanya usafi katika maeneo ya kutolea huduma za Umma na yale binafsi iwe endelevu,  tusisubiri mpaka tupewe shinikizo au kutokea matukio  bali tuifanye iwe tabia endelevu kwa usalama wa Afya zetu na wenzetu wanaotuzunguuka’’ amesema Kalli.

Maadhimisho hayo yametanguliwa na Mdahalo uliofanyika Desemba 8, 2023 uliolenga kuangazia mafanikio ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara, uliofanyika katika Ukumbi wa Kigoma Social Hall Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

Friday 1 December 2023

ZAIDI YA ASILIMIA 100 YA WAVIU WANATAMBUA HALI ZAO-DC MASALA

 

Posted On: December 1st, 2023

MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE KANALI MICHAELI MASALA AKIWASILI KWENYE ENEO LA HAFLA YA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KIMKOA ILIYOFANYIKA KIJIJI CHA SONGAMBELE WILAYANI BUHIGWE DESEMBA MOSI, 2023.BAADHI YA WAKAZI WA  WILAYA YA BUHIGWE WALIOJITOKEZA KWENYE KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI.

KAIMU MGANGA MKUU WA MKOA WA KIGOMA INNOCENT MSILIKALE AKITOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA UKIMWI KWA MKOA WA KIGOMA WAKATI WA KILELE CHA MAADHIMISHO HAYO AMBAYO KIMKOA YAMEFANYIKA KATIKA HALMASHAURI YA BUHIGWE.

Asilimia 119.4 ya wanaoishi na Virusi vya UKIMWI mkoani Kigoma wanatambua hali zao huku wakiendelea kudumisha ufuasi wa dawa za kufubaza na kupunguza makali ya maradhi hayo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Masala alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, ambayo kimkoa yamefanyika katika kijiji cha Songambele wilayani Buhigwe.

Amesema katika kupambana na kudhibiti maradhi hayo, serikali imefanikiwa kuanzisha vituo 93 vya kutolea tiba na mafunzo kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI ikiwa ni sawa na Asilimia 97.9 ya mahitaji halisi kwa mkoa.

Sambamba na hayo, katika kukabiliana na virusi vya UKIMWI, Kanali Masala ameitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya tatizo la kuongezeka kwa uzito uliopitiliza pamoja na kujenga tabia ya kupima Afya mara kwa mara hali, itakayosaidia kubaini maradhi katika hatua za awali ikiwemo ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.

Aidha Kanali Masala amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu imedhamiria kuyatumia maadhimisho hayo kwa lengo la kutoa Elimu, Hamasa pamoja na kuongeza ushiriki wa Asasi za kiraia katika kuhakikisha huduma za VVU na UKIMWI zinayafikia makundi mbalimbali kwenye Jamii.

Akitoa Taarifa ya hali ya utekelezaji wa Afua za UKIMWI kimkoa, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Innocent Msilikale amesema kuanzia Januari hadi Oktoba 2023, jumla ya watu 409,785 wamepima VVU na kati yao 4105 kugundulika na maambukizi ya UKIMWI ikiwa ni sawa na Asilimia 0.93 ya waliopima.

Amesema katika kukabiliana na maradhi hayo mkoa umeendelea kuhakikisha huduma za upimaji wa VVU zinapatikana wakati wote, kutoa huduma ya tohara kwa wanaume, kutoa dawa kinga, kusajili wateja wenye VVU, kutoa mafunzo kwa watoa huduma za Afya ili kuwajengea uwezo katika kutoa Elimu kwa jamii.

Aidha Msilikale amezitaja Changamoto zinazoendelea kukinzana na utekelezaji wa Afua hizo kuwa ni baadhi ya wateja kuacha matumizi ya dawa na kujikita katika tiba mbadala hali inayosababisha kuzorota kwa Afya zao na hata kusababisha vifo.

Wakazi mkoani Kigoma wametakiwa kushiriki katika kupinga ukatilia dhidi ya wanawake na watoto kwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya makundi hayo ili kufikia malengo ya usawa wa kijinsia.

Wito huo umetolewa Leo Novemba 28,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli alipozungumza akimwakilisha Mkuu wa Mkoa kuzindua Kampeni ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa Mkoa wa Kigoma.

Amesema waathirika wakuu wa madhara yatokanayo na vitendo vya ukatili wa kijinsia ni wanawake na watoto kutokana na jamii kutodhibiti tabia zisizozingatia usawa  wa kijinsia na haki za binaadamu kwa  makundi hayo.

‘’Tumeendelea kushuhudia vitendo vya utelekezaji wa familia, dhuluma katika mali za familia, ajira za watoto, unyanyasaji wa wanawake ndani ya ndoa pamoja na watoto wa kike kunyimwa haki zao za msingi katika familia na jamii kwa ujumla, mambo haya hayakubaliki na tunapaswa kuyapinga’’ amesema Kalli.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka wanawake kutosita kujitokeza na kutoa taarifa kwa uongozi na vyombo vya usalama pale wanapokabiliwa na madhila yanayohusisha aina yoyote ya ukatili wa kijinsia.

‘’Baadhi ya wanawake wamekuwa wakibakwa hususani wakiwa katika maeneo ya mashambani lakini kutokana na kuogopa kuaibika au kutopewa kipaumbele kwa changamoto zao katika jamii, huamua kukaa kimya jambo linalohatarisha usalama wao wa Afya ya mwili na Akili’’ amesisitiza Kalli.

Kupitia Maadhimisho hayo yaliyoanza kitaifa Novemba 25  hadi Desemba 10, 2023, Mkuu wa Wilaya amewasisitiza wataalam kuhakikisha wanafika na kufikisha ujumbe wa maadhimisho  katika maeneo yote ya mkoa wa Kigoma hususani vijijini ambapo vitendo hivyo vimekithiri.

Akiwasilisha taarifa ya shughuli zinakazofanyika katika siku 16 za maadhimisho, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kigoma Msafiri Nzunuri amesema lengo mahususi la maadhimisho hayo ni kuungana na wadau ili kupata nguvu ya pamoja katika kuhimiza na kushawishi jamii kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kufikia usawa.

Nzunuri amezitaja shughuli zinazofanyika kipindi cha kampeni ikiwa ni ufikishaji elimu na hamasa kupitia vyombo vya habari, kufanya mikutano na wananchi pamoja na kusikiliza kisha kutatua changamoto  zinazohusu ukatili wa kijinsia.

Aidha ameisisitiza jamii kuwekeza katika kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwa kuwa ni kundi ambalo linapitia changamoto nyingi ikiwemo mgawanyo wa majukumu katika familia, mila na desturi kandamizi, ukosefu wa ujuzi na umasikini.

Pia amebainisha changamoto nyingine zinazokabili kundi hilo ni  athari zitokanazo na changamoto za ubora na utoshelevu wa miundombinu nchini pamoja na ukubwa wa wategemezi katika kaya.

Kadhalika Nzunuri amesema matarajio ya Serikali pamoja na wadau ni kuhakikisha wanawake wanapata uelewa kuhusu masuala ya kijinsia, kupungua kwa idadi ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na jamii kufikia malengo ya usawa wa kijinsia.

Upande wake Katibu wa Kamati ya Maridhiano ya Dini mkoa wa Kigoma Padre Castus Rwegoshora amesema upande wao kama wahudumu wa masuala ya kiimani wanaendelea kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuheshimiana na kuchukualina  ili kudumisha hadhi na upendo kati ya wanadamu.

Pia ameishukuru serikali kwa kuendelea kutambua na kuchukua hatua dhidi ya changamoto ya uwepo wa vitendo vya ukatili miongoni mwa wanajamii.

Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, umehudhuriwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Elisante Mbwilo, wakuu wa Sehemu na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, viongozi wa Madhehebu ya Dini pamoja na wadau kutoka Taasisi za Umma na Binafsi.