Jumla
ya zana haramu za uvuvi 343 zenye thamani zaidi ya Shilingi za kitanzania
480,000,000 zimeteketezwa moto Mkoani Kigoma, ikiwa ni hatua ya Serikali ya
Mkoa kupambana na Uvuvi usioendelevu.
Zana
hizo zilikamatwa na vikosi vya doria ziwani kwa vipindi tofautitofauti katika
ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma.
Uvuvi
wa Kutumia zana haramu katika Ziwa Tanganyika umekuwa tishio katika Mwambao wa
Ziwa hilo ukiashiria kupoteza kabisa samaki na dagaa ambao ni kitoweo muhimu
kwa wakazi wanaolizunguka Ziwa Tanganyika na kwingineko.
Akiongea
wakati wa Zoezi la Uchomaji wa Zana hizo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw.
Charles Pallangyo alisema zoezi hili ni endelevu kwani Mkoa wa Kigoma
hautamvumilia Mtu yeyote kutumia zana za Uvuvi zisizo na tija katika kuendeleza
Uvuvi endelevu.
Pallangyo
amewataka wavuvi kufuata taratibu na sheria za matumizi ya zana za Uvuvi ili kulinda
Rasilimali za Ziwa Tanganyika kuwa endelevu kwa faida ya Vizazi vijavyo.
Naye
Afisa Uvuvi wa Mkoa wa Kigoma Bi. Ritta Mlingi amewatoa hofu wananchi wa Mkoa
wa Kigoma kuwa hakuna samaki anayevuliwa kwa sumu kama ilivyokuwa inavumishwa
na watu.
Aliongeza
kuwa zana za uvuvi zinapokamata samaki hupandishwa mtumbwini saa hiyohiyo
isipokuwa zana za “makila” ambazo huachwa hadi asubuhi ndipo huteguliwa na kupandishwa
kwenye chombo.
Hivyo
samaki wanaokamatwa mapema na “makila” hufa mapema kutokana na kukabwa sehemu
za mapezi “Gills” , kasi yake kwa kuharibika huwa ni kubwa uizingatia wavuvu
wengi hawana Barafu kwaajili ya kutunzia samaki ndani ya ziwa.
“Nawaomba
wananchi wasiwe na wasiwasi kwani samaki hawanasumu isipokuwa kukosekana nyenzo
bora za utunzaji pindi wanapovuliwa, hata hivyo mwanchi yeyote atakayekuwa na
ushahidi wa samaki mwenye sumu anakaribishhwa kuleta usahidi huo katika Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa” aliongeza Mlingi.
|
No comments:
Post a Comment