Thursday 12 December 2013

Wilaya ya Kakonko yajipatia shilingi 10,000,000 kwa kuibuka mshindi Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka Kitaifa 2013

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Lt. Col (Mst) Issa Salehe Machibya akipokeai Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Col.(Mst.) Fabian Massawe katika kijiji cha Kanyonza Wilayani Kakonko Wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Juni 2013.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Lt. Col (Mst) Issa Salehe Machibya akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2013 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mhe. Peter Kiroya muda mfupi baada ya kuupokea kutoka Mkoa wa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Lt. Col (Mst) Issa Salehe Machibya na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Col.(Mst.) Fabian Massawe wakipeana mawazo muda mfupi  mara baada ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Kanyonza Wilayani Kakonko Wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Juni 2013.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma /Ujiji Mhandisi Christopher Nyambele akicheza kwa furaha Wakati Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 zilipowasili katika Manispaa yake.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2013, Mhe. Juma Ali Simai akifungua rasmi Stenndi ya Mabasi ya Mkoa wa Kigoma iliyopo eneo la Mwasenga katika Manipaa ya Kigoma /Ujiji.
Picha zote na G.D. Ng'honoli- Afisa Habari wa RS Kigoma




Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013 zilihitimishwa katika Mkoa wa Iringa tarehe 14 Ocktoba 2013, ambapo Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma imejipatia zawadi ya shilingi 10,000,000 baadaya kuibuka mshindi wa kwanza katika  mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2013.
Akitangaza katika kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2013, Waziri wa Habari Utamaduni na michezo Mhe. Fenera Mkangara alieleza kila mwaka Mwenge wa Uhuru huzingatia vigezo vinavyopangwa kwa mwaka husika, na vigezo hivyo hushindanishwa kwa kila Mikoa,Wilaya na Halmashauri. Mwaka 2013 wilaya iliyofanya vizuri na kuibuka mshindi dhidi ya wilaya zote hapa Tanzania bara na Viziwani ni Wilaya ya Kakonko.
Wilaya ya kakonko ni mojawapo ya Wilaya tatu mpya zilizoanzishwa mwaka huu Wilaya ya Kakonko ikizaliwa na Wilaya mama ya Kibondo, sababu za Msingi zilizoifanya Wilaya hii kuibuka mshindi pamoja na uchanga wake ni kuwa na miradi bora iliyokamilika na inayowalenga wanchi moja kwa moja.
Baadhi ya miradi iliyozinduliwa na kuwekewa mawe ya Msingi katika Wilaya ya Kakonko ni pamoja na umeme, maji, afya na elimu. Mbio za mwenge wa uhuru zimekuwa kichocheo kikubwa kwa nchi katika kuhamasisha maendeleo mbalimbali ambapo miradi mingi imekamilishwa kwa nguvu za wananchi kuchangia fedha au nguvu kazi.
Sambaba na kuhamasisha manendeleo ya wananchi mwenge wa uhuru umeendeleza umoja, amani mshikamano wa watanzania.      






1 comment:

  1. Karibuni kaika blgo hii kupata habari mbalimbali za Mkoa wa Kigoma, Fursa za uwekezaji

    ReplyDelete