Monday 15 January 2018

SHULE SHIKIZI ZASAIDIA WATOTO KUPATA ELIMU MKOANI KIGOMA

Suala ala utoaji elimu si jambo la serikali tu bali ni ushirikiano wa sekta binafsi, jamii na serikali kwa pamoja zinaweza kuleta mabadiriko makubwa ya kimaendeleo kieleimu.
umbali kutoka maeneo wanayoishi jamii na sehemu inakopatikana huduma ya elimu imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya maeneo hususani vijiji ambapo jamii nyingi hasa za wakulima na wafugaji huishi kwa kuhamahama kufuata huduma za mashamba ya kilimo na malisho ya mifugo jambo amabalo hufanya jamii hizi zikae mbali na huduma za kijamii kama vile elimu, afya, usafiri.
Kijiji cha Kazage katika kata ya Shunguliba Wilayani Kasulu ni moja ya Kijiji ambacho kimepambana na  changamoto ya kuwa mbali na maeneo ya upatikanaji wa huduma za kijamii, suala lililopelekea watoto wengi kukosa fursa ya kupata elimu ya msingi.
Kijiji cha Kazage kipo umbali wa kilomita 10 hadi kufikia huduma ya elimu elimu ya msingi iliyopo katika kijiji jirani cha Shunguliba. Kutokana na umbali mrefu, asilimia 100 ya watoto wenye umri wa kwenda shule hushindwa kupata elimu.
Shirika la EQUIP Tanzania linalojishugulisha na mpango wa kuinua ubora wa elimu, ndilo limekuwa msaada katika kijiji cha Kizage kwa kuwaokoa watoto walioshindwa kupata elimu ya msingi likaja na mpango wa kusaidia uanzishwaji wa ‘Shule Shikizi’.
Shule shikizi zinatokana na shule mama zilizopotayari na zenye miundombinu kamili, shule hizi hujengwa ili kusaidi watoto waliokosa fursa ya masomo ya awali.
Kutokana na uhitaji wa elimu EQUIP Tanzania imeweza sasa kusidia ujenzi wa madarasa mawili ya shule shikizi katika kijiji cha Kizage, ujenzi wa madarasa mawili hadi sasa umesaidia watoto kupata elimu kwa asilimia.
Mtendaji wa Kijiji cha Kizage Bw. Timoth Zabronia anatoa ushuhuda wa faida za shule shikizi namna zilivyosaidia kuinua elimu kijijini hapo akisema “watoto wet hapa walikuwa wengi hawasomi kutokana na umbali mrefu hadi kuifikia shule mama iliyopo Kijiji cha shunguliba, sasa tunashukuru mradi wa EQUIP Tanzania kwa kuona umuhimu wa watoto wetu kupata elimu kupitia shule hizi shikizi sasa watoto wengi wameanza kupata elimu ya awali na hatimaye kuendelea na darasa la kwanza”
Wananchi wa Kizage wanato shukrani na pongezi kwa mradi wa EQUIP Tanzania ambayo imekuwa ikiwahamasisha kujenga maboma ya madarasa na kasha kusaidia hatua ya upauaji na samani za madarasa, kwa nguvu hii, wakazi wa Kizage wameweza kufyatua tofali kwa nguvu zao na kujenga madarasa mawili pamoja na ofisi ya walimu katika shule shikizi ili kuondokana na adha ya kukosa elimu watoto wao.

No comments:

Post a Comment