Tuesday 25 February 2014

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma awapatia Wakulima lita 200 za dizeli kwaajili ya Kilimo


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Luteni Kanali (Mst) Issa Salehe Machibya ametoa msaada wa lita 200 za mafuta ya dezeli ili ziwasaidie wakulima watakaokodisha Matrekita kwaajili ya shughuli za Kilimo katika Kijiji cha Sunuka Wilayani Uvinza.
Machibya ametoa msaada huo jana baada ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho ambapo walimwambia kuwa pamoja na kuwepo kwa bonde la Msombwe lililopo mita chache kutoka katika mto lugufu wamshindwa kulitumia vizuri bonde hilo kwa kukosa nyenzo bora za kilimo.
akitoa ahadi hiyo ya mafuta Machibya aliwaambia wakulima " nataka nione bonde hili linalimwa katika vipindi vyote kiangazi na masika kwani ni eneo zuri litawanufaisha na kuongeza kipato chenu" alisisitiza.
bonde hilo linafaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali kamavile mpunga, mahindi, alizeti, nyanya  na mbogamboga.
naye Kamanda wa Jeshi akimwakilisha Mkuu wa Kikosi cha JKT kambi ya Bulombora alisema wnanchi wanakaribishwa kukodi matrekta yaliyopo kambini hapo kwa bei nafuu ili waweze kuyatumia katika kukuza kipatao kupitia kilimo cha kisasa.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ni mwendelezo wa ziara zake ambazo amekuwa akizifanya kila mwezi katika wialya zote za Mkoa wa Kigoma kukagua hali ya wakulima na kufahamu mahitaji yao ili kuwawezesha  na kuwapatia wataalamu wa kilimo.

Mkuu wa Mkoa akipatiwa maelezo na Afisa Ugani wa Kijiji cha Sunuka Wilayani Uvinza.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali (Mst) Issa Machibya akitembezwa kukagua shamba la Mmoja wa wakulima katika kijiji cha kazuramimba wilayani Uvinza, mbele yake ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu . Hadijah Nyembo.

Moja ya Msafara wa Mhe. Mkuu wa Mkoa ukielekea kukagua mashamba ya Wakuima vijiji ya Kazuramimba na Sunuka Wilayani Uvinza.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Luteno Kanali (Mst) Issa Machibya akizungumza na Mkulima wa Nyanya katika kijiji cha Sunuka pembezoni mwa Mto Lugufu.

Mkulima wa zao la Mpunga akionesha mbegu ya mpunga iliyoathirika na ugonjwa ambapo aliomba msaada wa wataalamu wa kilimo ili kuweza kunusuru zao hilo.

Afisa Ugani akichukua maelezo ya Mkulima wa Mpunga juu ya ugonjwa unaoshambulia zao hilo kijijini hapo.

Kamada James kutoka kambi ya JKT Bulombora akizungumza na wanchi wa kijiji cha Sunuka namna ya kuomba kukodi matrekta kutoka katika Kambi ya JKT Bulombora.
 
Mkuu wa Mkoa akisalimiana na wakulima katika kijiji cha Sunuka muda mfupi mara baada ya kuwasili.


Habari na Picha -G.D. Ng'honoli (Afisa Habari wa RS Kigoma)

No comments:

Post a Comment