Sunday 10 December 2017

Nzunda awataka Maafisa Elimu kutenda haki kwa Walimu

W
atendaji wa Sekta  ya elimu Mkoani Kigoma, wametakiwa kutokuwa kisababishi cha kwanza kuwavunja moyo wafanyakazi walimu kwa namna yeyote bali wasaidine nao katika kuleta kuboresha na kuleta matunda bora kwenye sekta ya elimu.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye anashugulikia Elimu Tixon Nzunda ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Kigoma ambayo ililenga kukagua miradi mbalimbali ya elimu ikiwemo ukarabati wa shule kongwe pamoja na vyuo vya ualimu, kukagua miradi elimu inayofadhiliwa na wahisani mbalimbali namna inavyotekelezwa Mkoani Kigoma.











Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye anashugulikia Elimu Tixon Nzunda akipata maelezo ya ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Kigoma


Akiongea na wakurugenzi, maafisa elimu , waratibu wa elimu na walimu wakuu Nzunda aliwaambia kumekuwa na tabia ya watendaji kuwadhulumu walimu haki zao ikiwemo fedha za likizo, fedha za masomo kwa waliokatika mpango kadri ya mahitaji ya halmashauri, jambo ambalo limekuwa likiwakatisha taamaa na kuwavunja moyo waalimu.
“Mwalimu anakuja kwako wewe kama kiongozi wake na anashida za msingi kabisa lakini kutokana na sababu zako tu unamkwamisha, tusiwe vikwazo kuwakatisha tama walimu kwa kuwaonea kwenye haki zao bali tufungue milango kuwasikiliza na kuwapa ushauri Afisa elimu wa Halmashauri, kata na Mkuu wa Shule asiyejali waalimu wake huyu hafai kabisa kuwa kiongozi” aliongeza Nzunda.

Katibu  Tawala wa Mkoa wa Kigoma  Charles Pallango (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye anashugulikia Elimu Tixon Nzunda wakizungumza na uongozi wa wa Shule ya Sekondari ya Kigoma (hawapo pichani)


Nzuda amweataka watendaji kufanya kazi kwa uwajibikaji, uadilifu na weledi pamoja na kuwa wasikivu kwa kushughulikia matatizo ya umma.
Aidha suala la usimamizi thabiti wa miradi amesema lisiwe kwa sekta ya elimu peke yake bali miradi yote isimamiwe kikamilifu ili kuleta tija na maendeleo kwa wananchi.
Katika kukagua miradi ya ukarabati wa shule ya sekondari ya Kigoma Ndunda ameonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa wakala wa majengo Tanzania ambao unasuasua pamoja na kupewa fedha yote ya ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.



No comments:

Post a Comment