Zaidi ya watoto 16,448
sawa na asilimia 67.1
waliofaulu katika mtihani wa Taifa wa Darasa
la saba 2017 Mkoani Kigoma wataanza masomo ya kidato cha kwanza mapema Januari 2018
ikiwa ni wale waliochaguliwa kwa awamu ya kwanza.
Haya yametolewa na Afisa Elimu wa
Mkoa wa Kigoma Bw. Juma Kaponda katika kikao cha kutangaza matokea ya mtihani
wa Darasa la saba Mkoani Kigoma kilichofanyika mwishoni mwa mwaka 2017.
Jumla ya watahiniwa 36326
wasichana 18746 na wavulana 17580
ambao ni sawa na aslimia 99.25 ya wanafunzi walifanya mtihani wa kuhitimmu darasa la
saba Mkoani Kigoma mwaka 2017, ambapo kati yao waliofaulu kwa alama za
kuendelea na kidato cha kwanza ni 24,528 Wasicha 11,104 na wavulana 13,424.
Aidha wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 ni 16,448 sawa na aslimia 67.1 ya waliofaulu, hata hivyo wanafunzi
8080 sawa na asilimia 32.9 wamebaki bila kupangiwa shule wakisubiri hatua ya
uchaguzi wa awamu ya pili.
Mkoa umejiwekea mikakatai mbalimbali ikiwemo
kukamilisha vyumba vya madarasa, ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaweza
kuanza masomo mapema kabla ya Februari. Mkoa wa Kigoma umeshika nafasi ya 18
Kitaifa katika ufaulu wa Mtihani wa darasa la saba.
No comments:
Post a Comment