Friday, 21 February 2014

Wafanyabiashara watakiwa kutojihusha katika rushwa kama njia ya kukwepa kuipa kodi





Wafanyabiashara watakiwa kutojihusha katika rushwa kama njia ya kukwepa kuipa kodi





Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi Dkt. John Ndunguru akitoa Maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kigoam (Hayupo pichani) katika kikao alichokiitisha kwa lengo la kupeana taarifa juu ya Ulipaji kodi na Matumizi ya Mashi za Kielektroniki ambazo wafanyabiashara wanatakiwa kuanza kuzitumia.
Dkt. Ndunguru akisisitiza jambo katika kikao cha wafanyabiashara na Uongozi wa Mkoa wa Kigoma kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Ofisi ya  Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma


Wafanyabiashara wa mji wa Kigoma wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Dkt. John Ndunguru wakati wa kikao cha wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa kiichofanyika jana katika Ukumbi wa Ofisi ya Katibu Tawala  wa Mkoa wa Kigoma

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi Dkt. John Ndungurua amawatahadharisha wafanyabiasha kutojihusisha na rushwa kama mbinu ya kukwepa ulipaji wa kodi wanapofikiwa na maafisa wa Mamlaka ya Mapato Mkoani Kigoma.

Dkt. Ndunguru ameyasema hayo wakati wa kikao maalumu alichokiitisha kati yake na wafanyabiahsra pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kigoama kufuatia malalamiko na mgogoro wa baadhi ya wafanyabiashara kufungiwa maduka yao baada ya kugomea utaratibu wa Matumizi ya mashine za kuuzia za kielektroniki EFD (Electronic Fiscal Divices) uliowekwa na Serikali.

Akizungumza na wafanyabiashara Dkt. Ndunguru alielezwa kuwa baadhi ya maaofisa kutoka Ofisi ya Mamlaka ya Mapato mkoani Kigoma wamekuwa wakiwafuata wafanyabiashara na kuwaomba fedha kidogo ili wawapunguzie makadirio ya kodi jambo ambalo limelesababisha migogoro na chuki kati ya Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kigoama. 
Aidha Dkt. Ndunguru amemwagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kigoma afuatilie watumishi wanaosemekana kujihusisha na unyanyasaji wa wafanyabiashara na wale wasiozingatia maadili ya utumishi wa umma waweze kupewa onyo kali.
" Ofisi ya Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kigoma inatakiwa ifanye mikutano na wfanyabiashara au uongozi wa wafanyabiashara ili kupeana habari mbalimbai kwni migogoro mingine inatokana na kutokuwa na taarifa sahaii" aliongeza Dkt. Ndunguru.

Habari na Picha -G.D. Ng'honoli (Afisa Habari wa RS Kigoma) 

No comments:

Post a Comment