Baadhi ya Wacheza ngumi katika timu ya Mkoa wa Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mkoa wa Kigoma |
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akimpongeza Binti ambaye alishiriki katika kuiinua timu ya ngumi wakati wa mashinda ya ngumi ya kumuenzi hayati Nelson Mandela yaliyofanyika mwezi huu Jijini Dar es Salaam |
Timu ya Masumbwi ya Mkoa wa Kigoma
yaibuka nafasi ya Pili Kitaifa
Timu
ya Ngumi ya Mkoa wa Kigoma imeibuka mshindi wa pili kitaifa katika mashindano
ya ngumi yaliyofanyka
tarehe 5 Februari 2014 jijini Dar es Salaam
Mashindano
hayo yalilenga kumuenzi hayati Nelsoni Mandela ambaye aliyekuwa mwanamasumbi
mahiri na rais wa kwanza mweusi wa nchini ya
Afrika ya Kusini.
Akikabidhi
vikombe kombe viwili vya fedha na dhahabu Mwenyekiti wa Timu ya Ngumu Mkoa wa
Kigoma Bw. Iddie Kikwesha alisema vijana wapatao 10 wakiwemo wasichana 3 na
wavulana 7 wamejipatia medali 9 zikiwemo medali 3 za dhahabu 4 za fedha na 2 za
shaba.
Bwana
Kikwesha aliongeza kuwa kati ya ashiriki kumi mshiriki mmoja Bw. Ezra Paul
amechaguliwa kuungana na vijana wengine kuunda timu ya Taifa itakaoyoshiriki
mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Mwezi Machi 2014 nchini Uturuki, smbamba
na hilo washiriki wengine 9 wamchaguliwa kuingia katika timu ya taifa ya ngumu.
Kufuatia
ushindi huo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya
amewapongeza wanamasumbi hao kwa wameuletea sifa na heshima Mkoa wa Kigoma, naye Katibu Tawala wa Mkoa
Mhandisi Dkt. John Ndunguru ametoa rai kuwa atasaidiana na wadau mbalimbali
katika kukuza wigo wa michezo mbalimali ili kuuwezesha mkoa kuwa na nafasi
nyingi za ushindi katka michezo pia kama njia ya kuutangaza na kuvutia
wawekezaji.
Habari na Picha zote -G.D. Ng'honoli (Afisa Habari wa RS Kigoma)
No comments:
Post a Comment