Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Eng. Dkt. John S. Ndunguru akitoa hotuba kwa wananchi wilayani Uvinza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya lishe Kimkoa. |
Eng. Dkt. John Ndunguru abaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma akitoa matone ya Vitamini A kama shughuli mojawapo ya kampeni ya lishe. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw. Hamis Betese akishiriki kucheza ngoma ya asiliiliyoutumbuizwa na kikundi cha Mapigo Tisa. |
Mkoa wa
Kigoma umezindua rasmi leo kampeni ya lishe ki-Mkoa Kufuatia agizo la Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete alilolitoa siku ya Uzinduzi wa kampeni ya lishe kitaifa Mwezi mei, 2013, kwamba kila Mkoa ufanye uzinduzi wa kampeni hiyo.
Akiwahutubia
wananchi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi Dkt. John Ndunguru kwa niaba
ya Mkuu wa Mkoa ameziagiza Halmashauri ziwe na mpango wa lishe wenye kutoa
matokeo chanya kwa muda mfupi kwa
kutumia Rasilimali zinazopatikana Mkoani Kigoma.
Bado Serikali
inaendelea kukabiliana na changamoto ya uelewa mdogo wa wananchi kuhusu masuala
ya lishe katika jamii, kuanzia ngazi ya familia hadi kwa watendaji; ametaja baadhi
ya visababishi vya utapiamlo ni ulaji duni na mbaya, maradhi mbalimbali,
kutokuwa na uhakika wa chakula matunzo duni ya mama na mtoto, mazingira
machafu, umaskini wa kipato na baadhi ya sera zisizotambua umuhimu wa lishe kwa
maendelo ya nchi yetu.
Aidha ametoa
wito kwa kwa wasanii, waandishi wa habari kutumia nafasi walizonazo katika
kuielimisha jamii juu ya lishe ili kuisaidia Serikali kuboresha lishe kwa
wananchi, elimu ya lishe izingatie uzalishaji na ulaji wa vyakula mchanganyiko.
Dkt.
Ndunguru amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi nyingi za Afrika kwa kuwa
na kiwango kikubwa cha utapiamlo unaohatarisha ustawi wa watoto, mama
wajawazito na maendeleo ya kiuchumi na Kijamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment