Thursday, 20 March 2014

Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Dkt. John Ndunguru atembelea Mradi wa Ujenzi daraja la Malagarasi (Daraja la Kikwete) na Ujenzi wa Barabara ya Kigoma -Tabora

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Eng. Dkt. John Ndunguru akikagua mradi unaomalizika wa Ujenzi wa Daraja la Kikwete lililopo mto Malagarasi Mkoani Kigoma.
Mradi wa ujenzi wa daraja la “Kikwete” katika bonde la Mto Malagarasi 275m na barabara ya kilometa 48 kwa kiwango cha lami umekamilika kwa 95%
 Gharama ya Mradi ni USD: 56 milioni.  Muda wa mradi ni miezi 36, mradi ulikamilika tangu mwezi Desemba 2013.  Chanzo cha fedha ni Benki ya Korea na Serikali ya Tanzania kwa upande wa fedha za ndani.
Mkandarasi ni Kampuni ya Hanil Engineering na Mhandisi Msimamizi ni CHEIL Engineering zote kutoka Jamhuri ya Korea.  
Sehemu ya Daraja la Kikwete mto Malagarasi kwa mwonekano wa juu.

Mkandarasi akitoa maelezo ya kuhusu mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kigoma -Tabora kwa Kiwango cha lami.

Meneja wa wkala wa Barabara (mwenye shati jeupe) akifafanua jambo kwa Mkandarasi wa mradi wa Ujenzi wa barabar a ya Kigoma -Tabora kwa kiwango cha lami.

Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara na Daraja la Kikwete akielezea hatua za miradi hiyo wakati Katibu Tawala wa Mkoa alipotembelea mradi huo.



Mkoa una jumla ya Km 3,106 za barabara ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo:-  Barabara kuu ni km 663, barabara za mkoa 446 na barabara za vijiji ni km 1997,  barabara zote ni za udongo au changarawe. hadi sasa Mkoa wa Kigoma una jumla ya zaidi ya km 200 za barabara zenye kiwango cha lami. Barabara hizi ni barabara ya Kigoma-Kidahwe (37km), Mwandiga-Manyovu (60km), sehemu ya Kidahwe-Uvinza (76km), na (48km) barabara za daraja la Kikwete zilizopo hatua ya mwisho.


Mradi wa ujenzi wa barabara ya Kidahwe – Uvinza (76.6km) kwa kiwango cha lami unaendelea vizuri.  Mpaka sasa kilometa 70 za lami zimekamilika, Kalvati zote zimekamilika pamoja na madaraja mengine madogo (Box Culverts) na daraja kubwa la Mto Ruchugi. Kwa ujumla utendaji wa kazi mpaka sasa ni  98%.
Gharama za mradi ni Shilingi 78,241.102 milioni na ulikamilika mwezi Oktoba 2013.  Mradi huu unafadhiliwa na Mfuko wa Abu Dhabi ikishirikiana na Serikali ya Tanzania. Mkandarasi wa ujenzi ni Kampuni ya CHICO kutoka China na Mhandisi Mshauri ni Kampuni ya International Consultants and Technocrats Pvt Ltd kutoka India.
 
Sehemu ya Barabara ya Kidahwe – Uvinza iliyokamilika kwa kiwango cha Lami.





No comments:

Post a Comment