Michikichi
ni zao mojawapo ya mazao ya mafuta ambalo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya
Kigoma, Mbeya na Tanga hapa nchini Tanzania. Aidha zao hili hulimwa pia kwa
kiasi kidogo katika mikoa ya Kagera, Pwani, Rukwa, Morogoro na visiwa vya Pemba
na Unguja. Mkoa wa Kigoma ukiwa ni eneo
muhimu kwa uzalishaji wa zao la michikichi hapa Tanzania kwa mwaka huzalisha
zaidi ya tani 2,000 za mawese na zaidi ya tani 450 za mafuta ya mise.
Zao la mchikichi limekuwa
mkombozi kwa wakulima wengi wa Mkoa wa Kigoma kwani hutumika kwa chakula, biashara,
mafuta ya mise hutumika katika mapishi ya vyakula mbalimbali pia husaidia mwili
kupata nguvu na joto na hutumika katika
utengenezaji wa sabuni na vipodozi mbalimbali.
Hata hivyo nchi za Indonesia na Malaysia ambazo zilitoa mbegu ya zao la mchickichi kutoka Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania miaka ya 1960 kwa sasa zinaongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa mafuta ya mawese na bidhaa zitokanazo na michikichi.
Malysia pekee huzalisha
tani milioni 18.79 million za mafuta ya mawese na kusambaza tani milion 18 za mazao yanayotokana na zao la michikichi duniani yakiwemo mafuta ya mawese ambayo Tanzania imekuwa ikiagiza takribani asilimia 65 ya mafuta
ya mawese kutoka nchini ya Malaysia, zikifuatiwa na nchi nyingine kama Kolumbia
na Thailand.
Kwa ukanda wa Afrika
nchi za Nigeria, Kenya, Ghana, Cameroon na Benin zinatajwa kuongoza katika
uzalishaji wa zao la mchikichi ambapo nchi ya Naigeria huzalisha tani milioni
2.3 ya mafuta ya mawese kwa mwaka na kuifanya kuwa nchi ya tatu kwa uzalichaji
kidunia.
Matunda ya michikichi yakiwa yanaandaliwa kwa kukaushwa juani. |
Kiasi hiki ni kingi
ukilinganisha na fursa na uaptikanaji wa zao hili nchini Tanzania hususan Mkoa
wa Kigoma haipo katika rekodi ya
uzalishaji. Sababu kubwa zinazofanya zao hili kutojulikana na hata kutomnufaisha
mkulima wa kawaida nchini Tanzania ni teknolojia duni ya kilimo cha zao hili na
ukosefu wa miunndombinu ya kuchakata mazao yatokanayo ya mchikichi hususan
viwanda.
Kwa upande mwingine
wataalamu wa kilimo hawajaweza kutilia maanana juu ya umuhimu wa zao hili,
Serikali nayo haijawea kipaumbele namna ya kutoa ruzuku kwa wakulima wa zao la
mchikichi ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Wakulima wakiandaa matunda ya michikichi baada ya kuyatoa shambani. |
Kadhalika bidhaa mathalani
vile mapaa ya ndani (ruffing Materials) ambayo hutokana na makapi ya mchikichi
huingizwa kwa wingi nchini kutoka Malaysia, na Afrika ya Kusini. Wakulima wa
zao hili wengi hutumia zana duni katika kuchakata mazao ya michikichi kiasi ambacho
hakiwapi tija kukuza uchumi. Sambamba na ukosefu wa zana za kilimo nguvu ya
serikali kupitia wizara ya Kilimo ingeweza kufikiri namna ya kuwashirikisha
wadau wa maendeleo, mashirika binafsi ili kushawishi uwekezaji katika zao la
mchikichi kwa Kuweka miundombinu kama nishati ya umeme kwaajili ya kujenga
viwanda.
Moja ya njia za kiasili zinazotumika katika kuchakata na kuchuja mafuta ya Mawese mkoani Kigoma. |
Kwakuwa zao hili hutoa malighafi zaidi ya tatu ingekuwa fursa kwa wakulima kutengeneza wigo wa upatikanaji wa biashara za mazao ya mchikichi kama vile vipodozi, vyakula vya mifugo, sabuni na mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine nyingi kadha wa kadha.
Serikali kwa kutumia
wataalamu wake katika ngazi mbalimbali ikiwemo Halmashauri, na ngazi mbalimbali
za uongozi hazina budi kushirikiana na mashirika mbalimbali ya maendeleo katika
kuhakikisha kuwa zao la michikichi linakuwa moja ya mazao makuu katika kukuza
kipato na kuwaondolea umaskini wananchi wa mkoa wa Kigoma.
Nitapata wapi mbegu bora za michikichi?
ReplyDelete