Mkuu wa Mkoa wa Rutana Mhe. Juvenali Ndayiragije kutoka nchini Burundi amesifia jitihada za serika ya Tanzania katika Ujenzi na upanuzi wa Uwanja wa Ndege Mkoani Kigoma ambao kwa kiwango kikubwa umekuwa msaada kwa abiria wa Burundi kuutumia katika safari malimbali ndani na nje ya Afrika.
Mhe. Ndayiragije amesema hayo wakati alipotembelea kiwanja cha ndege cha Mkoani Kigoma jana, ambapo alifuatana na wakuu wa wilaya, Maafisa washauri katika ngazi mbalimbali Mkoani Rutana.
Naye Meneja wa Kiwanja cha Ndege Mkoani Kigoma aliwaeleza waviongozi hao kuwa ni vema sasa wakawahimize wananchi wao kutumia uwanja wa ndege wa Kigoma ambao upo karibu.
Sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma inayoonekana ni njia ya Kutua na Kurukia ndege. |
No comments:
Post a Comment