Jumla ya Tsh. 32 Bilioni zitatumika katika mradi Mkubwa wa Maji Mkoai Kigoma katika Maispaa ya Kigoma Ujiji mradi unasimamiwa na Kampuni ya Specon Ltd. , fedha hizo ikiwa ni msaada kutoka chi za jumuiya ya Ulaya pamoja na nguvu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
Hatua za kusukwa nondo za tanki la maji eneo la Mjimwema karibu na Ziwa Tanganyika |
Mradi huu utahusisha ujenzi wa matanki makubwa ya Maji yeye ujazo wa lita 2,000,000 za maji kilamoja yatakayojegwa katika maeneo tofauti dai ya maispaa ya Kigoma/Ujiji, (Mnarani na Mjimwema).
|
Baadhi ya Wataaalamu kutoka Ofisi ya Mamlaka ya Maji Kigoma Wakikagua maedeleo ya mradi wa maji. |
Kukamilika kwa mradi huu kutapunguza shida ya upatikanaji wa Maji katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa 95%. Aidha, sambamba na ujenzi wa matanki hayo kutakuwa na ujenzi wa matanki mengine 16 pamoja na kutandaza mabomba ya kupitishia maji urefu wa 16.6 km. .
|
Wafanyakazi wakiwa katika hatua ya kumwaga jamvi la moja ya matanki ya maji. Mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi, 2015. |
No comments:
Post a Comment