Wanafunzi wa Shule ya Msingi Businde pamoja na walimu wakitembezwa na Afisa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bi. Dorah Buzaire walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma kwaajili ya mafunzo ya somo la Uraia yaliyolenga Mada ya kufahamu Muundo wa Serikali ya Mkoa na namna jinsi ofisi hiyo inavyofanya kazi na wanchi.
Afisa Utumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bi. Zainabu Mbunda akitoa maelezo namna Ofisi ya Mkoa inavyofanya kazi pamoja na muundo wake kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Businde (hawapo pichani ) walipofika kujifunza juu ya mada hiyo.
Baadhi ya wanafunzi waliofika kujifunza wakifuatilia Mada kutoka kwa Afisa Utumishi wa Mkoa (hayupo pichani).
No comments:
Post a Comment