Tuesday, 4 March 2014



Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Kanali (mst) Issa Machibya akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Kijiji cha Sunuka wakati alipotembela kijijini hapo mapema mwezi huu.

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo akitoa  ufafanuzi wa masuala  ya Elimu kwa viongozi wa Kijiji cha Sunuka wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Mkoa Luteni Kanali (mst.) Issa Salehe Machibya ameanza kuwachukulia hataua za kisheia wazazi ambao hawakuwapeleka watoto wao waliofaulu  kuanza kidato cha kwanzamwaka 2014.
Machibya ameyasema haya wakati wa Ziara ya Mkoa mzima anayoifanya kufuatilia masuala ya Elimu;akiwa katika Wilaya ya Uvinza kijiji cha Sunuka  alisema " wazazi wote wasiopeleka watoto waliofaulu kidato cha kwanza 2014 watachukuliwa hatua kali za kisheria zoezi hili nila Mkoa mzima".
Hivi karibuni imeripotiwa kuwa karibu  60% ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwnza mwaka 2014 hawajaripoti, baadhi ya sababu zinazoelezwa ni ukosefu wa fedha (umaskini), baadhi ya wazazi kuwaozesha mabinti, na kuwafanya wengine kama sehemu ya kujipatia kipato kwa kuajiriwa kwa kazi za shambani ndani na nje ya mkoa wa Kigoma.
Machibya alisema hatomwelewa mzazi yeyote kwa sababu kama hizo kwani Mkoa umejaiwa kuwa na hali ya hewa nzuri na udongo wenye kuzalisha kila aina ya Mazao.

No comments:

Post a Comment