Balozi wa Ujerumani
Nchini Tanzania awasili Mkoani Kigoma kwa ziara Maalumu.
Uzalishaji wa asali na nta
Mkoani Kigoma umeongezeka kutoka tani 100 za asali na tani 5 za nta mwaka 2007
hadi kufikia tani 346 za asali na 10 za nta mwaka 2013, ongezeko hili limesaidia
kuinua kiwango cha mauzo ya wafugaji nyuki kutoka Shs. 315 milioni mwaka 2007 hadi Shs. 2.14 bilioni mwaka 2013.
Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Adam Koenraad akigawa kadi za Mawasiliano binafsi kwa wenyeji wake mara
baada ya kuwasili jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
|
Mafanikio haya yanatokana
na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana
na Serikali ya Ubelgiji ambapo mradi wa kuendeleza ufugaji Nyuki umeboresha
uchakataji, na kutafuta masoko ya asali,
nta na mazao mengine ya nyuki katika Wilaya za Kibondo na Kigoma ambapo jumla
ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia saba (1,700,000,000/=) zilitolewa na Serikali
ya Ubelgiji kusaidia mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali (mst.)
Issa Machibya akitoa hotuba ya ukaribisho wakati Balozi wa Ubelgiji Nchini
Tanzania alipotembelea Ofisini kwake jana asubuhi.
|
Balozi
wa Ubelgiji nchini Tanzania Bw. Adam Koenraad akielezea namna nchi yake inavyopanga kushirikiana na
Tanzania hususan Mkoa wa Kigoma katika masuala mbalimbali ya maendeleo kwa
wananchi.
|
Viongozi mbalimbali katika Sekretariati ya Mkoa wa Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania watatu kutoka kushoto |
No comments:
Post a Comment