|
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufungua kikao
cha wadau wa TIKA Mkoani Kigoma. |
|
Wajumbe wa Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Tiba kwa Katika uliofanyika jana Katika Ukumbiwa NSSF Mkoani Kigoma. |
Manispaa ya
Kigoma/Ujiji katika Mkoa wa Kigoma imetakiwa kuanza kutekeleza mpango wa afya ya Tiba kwa kadi (TIKA) kwa wananchi
wake kwa kutoa elimu na uhamasishaji kwa wananchi ili wajiunge na mpango huo.
Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Hadijah Nyembo aliposoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma katika kikao cha wadau waMfuko wa Tiba kwa Kadi(TIKA) uliofanyika katika Ukumbi wa NSSF Mkoani Kigoma.
|
Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Bw. Moses D. Msuluzya akitoa neno kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma wakati wa Kikao cha wadau wa TIKA. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe. Yahya E. Nawanda akitoa uzoefu wa uendeshaji wa TIKA na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Tiba kwa Kadi. |
Akitoa uzoefu wa uendeshaji wa Mfuko wa huduma za Afya vijiji Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Yahya E. Nawanda aliaambia viongozi wa siasa na dini washikamane ili kuhamasisha wananchi kujiunga na mifuko hii bila kujali itikadi ya vyama, rangi, au dini kwani magonjwa na kifo haichagui hayo yote.
Aidha amewataka watendaji wa ngazi zote kuwajibika kwa wananchi ili kuwaletea unafuu wa gharama za matibabu kwa kuwahamsisha wananchi kujiunga na kuchangia fedha kidogo katika mifuko hiyo.
TIKA ni mfumo wa
utoaji wa huduma za afya kwa gharama nafuu inayowalenga wanajamii waliopo
katika sektazisizo rasmi maeneo ya Mijini, huduma hizo ni pamoja na Upatikanaji
wa dawa na vifaa tiba kwa gharama nafuu.
|
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe. Yahya E. Nawanda (katikati) akisikiliza kwa makini hoja za wachangiaji mara baada ya kutoa uzoefu wa uendeshaji wa TIKA na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Tiba kwa Kadi, kushoto ni Mhe. Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Iddi Ruhomvya na kulia ni Bw. Moses D. Msuluzya Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. |
|
Viongozi mbalimbali wa Mfuko wa huduma za Afya NHIF wakiandika Maswali na hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wadau wa TIKA wakati wa kikao hicho. |
|
Mshiriki wa kikao cha wadau wa mfuko wa Tiba kwa Kadi
(TIKA) wakichangia hoja wakati wa majadiliano ya kikao hicho
kilichofanyika katika Ukumbi wa NSSF Mkoani Kigoma. |
|
Washiriki wa kikao cha wadau wa mfuko wa Tiba kwa Kadi (TIKA) wakichangia hoja wakati wa majadiliano ya kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa NSSF Mkoani Kigoma. |
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Kidani Magwilla Matibabu ya mpango wa
TIKA yanalenga kuhudumia kaya, Taasisi,na Vikundi ambapo kwa ngazi ya kaya Baba
, mama na watoto wasiozidi umri wa miaka 18 watachingia kwa gharama zitakazokubalika kama
gharama ya matibabu kwa mwaka mzima na kila mwanachama atapatiwa kadi itakayomwezesha
kutibiwa katika vituo mbalimbali vya afya vitakavyounganishwa na utaratibu wa
tiba kwa mwaka mzima.
No comments:
Post a Comment