Sunday, 15 June 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA UCHANGIAJI DAMU YAFANYIKA MKOANI KIGIOMA

Makundi mbalimbali yakiwa katika maandamano ya maadhimisho siku ya Uchangiaji damu iliyofanyika Mkoani Kigoma. 

Makundi mbalimbali yakiwa katika maandamano ya maadhimisho siku ya Uchangiaji damu iliyofanyika Mkoani Kigoma. 

Mama Salma Kikwete akikagua mabanda ya maonesha katika uwaja wa Lake Tanganyika siku ya maadhimisho ya Uchangiaji damu iiyoadhimishwa Ktaifa Mkoani Kigoma.

Wananchi wakijitokeza kuchangia damu wakati wa maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Kigoma.

Mgeni rasmi akipewa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mpango wa Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS).


Moja ya makundi mbalimbali yaliyojitokeza katika maandamano siku ya maadhimisho ya uchangiaji damu iliyofanyika kitaifa Mkoani Kigoma.

Kikundi cha ngoma kutoka nchi ya Burundi kikitoa burudani katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu Kitaifa katika uwanja wa Lake tanganyika Mkoani Kigoma.

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya damu salama Mhe. mama Salma Kikwete akizindua mfumo wa kielektroniki wa kutunza kumbukumbu za wachangiaji damu uliotolewa kwa msaada wa nchi ya Marekani.

Mkuu wa wilaya ya Kibondo Bw. Venance Mwamoto akipokea cheti cha utambuzi katika kuhamasisha uchangiaji damu ambapo vyeti hivyo vilitolewa kwa Wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Kigoma.

Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Afya ambay pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Leonard Subi akionesha Cheti ambacho kilitolewa na MPANGO wa Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS) kama ishara ya kutambua mchango wake katika kufanikisha Mkoa wa kigoma kuvuka lengo la uchangiaji damu kutoka chupa 3,000 na kufikia hadi chupa 3,620

No comments:

Post a Comment