Miundo
Mbinu ya Kisasa kuufanya Mkoa wa Kigoma Kitovu cha Kibiashara kwa nchi za
Burundi na Congo DRC.
Uchumi wa taifa lolote
duniani hutegemea ubora wa miundominu iliyopo katika sekta mbalimba inanazowezesha
biashara na uwekezaji, miundombinu bora na ya kisasa inahitajika katika nchi
yetu ili kuweza kushawishi uwekezaji wa ndani na nje mathalani uwepo wa Barabara,
viwanja vya Ndege, bandari na nishati ya umeme.
Eneo la maegesho ya
meli katika Bandari Mkoani Kigoma eneo hili hupokea meli za mizigo na abiria
kutoka nchi za Burundi , Kongo na Zaire.
|
Jenereta za kisasa za kuzalisha Umeme mjini Kigoma.
|
Hayawi hayawi sasa
yamekuwa ni msemo wa enzi na enzi wenye kuamsha shauku ya kile kilichongojewa
kutimia, ndivyo ilivyo kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma ambao kila mmoja bila
kujali itikadi aliyonayo kisiasa anakiri wazi tena hadharani nguvu na kasi ya
kimaendeleo inayofanywa na Serikali ya awamu ya nne chini ya Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete kubadili sura ya Mkoa na kuondoa
habari za kihistoria za ubovu wa
Miundombinu ya Mkoa huu.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
Mhe. Luteni Kanali (mst) Issa Salehe Machibya anathibitisha kwa kusema miundo mbinu katika Mkoa wa Kigoma
imeimarika kwa zaidi ya asilimia 85.
Uwanja wa ndege Mkoani Kigoma baada ya kufaanyiwa maboresho na upanuzi. |
Uwanja wa ndege Mkoani Kigoma kabla ya kufanyiwa upanuzi na maboresho. |
Hapo nyuma tangu uhuru Mkoa wa Kigoma kwa
upembeni wake katika sura ya Tanzania ulikuwa nyuma katika suala zima la maendeleo
kwa kukosa kabisa Miundombinu bora kama vile Barabara, bandari, usafiri wa
anga, miundo mbinu hii si kwama haikuwepo bali ilikuwepo lakini iliuwa na
kiwango duni kiasi cha kutowezesha mawasilano na usafiri wa haraka kirahisi kwenda
Mikoa mingine.
Ni
dhahiri kabisa kuwa usumbufu huo sasa unaelekea
kukoma na kutokomea mara baada ya serikali ya awamu ya nne kugeuzia
jicho lake katika Mkoa wa Kigoma, ambapo zaidi ya kilomita 200 za Barabara
zimejengwa kwa kiwango cha lami Barabara zilizizokuwa na usumbufu kama vile Mwandiga – Manyovu (kilomita 60); Kigoma –
Kidahwe (kilomita 35.7) na Kidahwe – Uvinza (kilomita 76.6).
Ujenzi wa Barabara ya
rami Kidahwe – Uvinza (kilomita 76.6) inayounganisha Mkoa wa Tabaora na Kigoma.
|
Aidha ujenzi wa daraja la Kikwete katika mto
Malagarasi lenye urefu wa mita 275 pamoja na kuinua tuta la bonde la mto
Malagarasi lenye urefu wa kilomita 2 umekamilika, Ujenzi wa daraja hilo
unaambatana na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami pande zote mbili za
daraja (approach roads) zenye urefu wa kilomita 48. Kufungua kwa daraja hili
kutaunganisha Mkoa wa Kigoma na Mkoa jirani wa Tabora ambayo ndiyo njia kuu
katika kuunganisha na Mikoa mingine Tanzania.
Mhe. Machibya
anaeleza moja ya faida za kukamilika kwa daraja la Mto Malagarasi alimaarufu
Daraja la Kikwete kuwa litatoa wigo mkubwa kwa Mkoa wa Kigoma kuwasiliana na
mikoa mingie kiurahisi, wafanyabiashara wa mazao ya kilimo kama vile miwa,
nanasi, ndizi sasa wanauwezo wa kusafirisha mazo hayo kwenda mikoa jirani ya
Tabora na kwingineko kwa uharaka na muda wote wa misimu bila kukwama.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma (wa pili toka kushoto) Eng.
Dkt. John S. Ndunguru akikagua moja ya Shughuli za ujenzi wa Barabara Mkoani
Kigoma
|
Daraja la Kikwete
katika mto Malagarasi lenye urefu wa mita 275 ambalo limekamilika.
|
Daraja la Kikwete
katika mto Malagarasi lenye urefu wa mita 275 ambalo limekamilika.
|
Maeneo mengine ya
miundombinu kama vile ya Reli, Bandari na Uwanja wa Ndege navyo
havijasahaulika. Kwa mfano, Uwanja wa Ndege wa Kigoma, ambao umefanyiwa upanuzi
kutoka mita 30 hadi 45 za sasa ili kuwezesha Ndege kubwa za abiria na mizigo
kutua mkoani Kigoma.
Naye Mhandisi Dkt. John
S. Ndunguru ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kwa shauku anelezea namna
Mkoa wa Kigoma unavyojipanga katika kutumia fursa ya Nchi jirani za Burundi na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambazo kwa kiwango kikubwa zinategemea sana
upitishaji wa mizigo yake kupitia Tanzania Mkoani Kigoma. Aidha wasafiri
watakaotumia Uwanja wa Ndege wa Kigoma kutoka nchi hizo wataongezea maradufu. Kukamilika
kwa miundo mbinu hii ni ishara wazi kuwa Mkoa wa Kigoma unafunguka na kuwa
kitovu cha kibiashara.
Baadhi ya wakazi wa
Mkoa wa Kigoma wamekuwa wakikiri wazi kuwa Kigoma ya sasa si yazamani ambapo
reli ya kati ndiyo pekee ilitegemewa kwa usafiri na usafirishaji, imani yao kwa
sasa ni kwamba Miundombinu iliyowekwa sasa imeufungua mkoa wa Kigoma na fursa
nyingi zimeanza kuonekana katika sekta ya kilimo na mifugo, Uvuvi, utalii
pamoja na uwekezaji katika eneo Maalumu la Kigoma “Kigoma Special Economic
Zone”.
Shughuli za Uvivi
hufanywa na wakazi wa Kigoma katika Ziwa Tanganyika ambapo samaki na dagaa
husafirishwa kwa wingi kwenda nchi jirani za Kongo na Burundi
Shughuli za Uvivi
hufanywa na wakazi wa Kigoma katika Ziwa Tanganyika ambapo samaki na dagaa
husafirishwa kwa wingi kwenda nchi jirani za Kongo na Burundi
|
Mhandisi Dkt. Ndunguru
anafafanua kuwa jambo ambalo kwa sasa wanaihiaji wanakigoma sambamba na
kuendelea kukamilishwa kwa mawasiliano ya Barabara, na Uwanja wa Ndege, kiu
kubwa iliyopo mbeleni ni kukamilishwa kwa masoko ya mpakani katika maeneo ya
Muyama (Wilayni Buhigwe) Mkarazi(Wilayani Kibondo) na Kagunga( Wilayani Kigoma)
mwambao wa ziwa Tanganyika ambako soko la Kimataifa linajengwa.
Zipo biashara zisizo
rasmi zinazofanywa na wanchi wa Tanzania na Burundi hasa waishio mpakani ambazo
kimsingi hazina tija katika kukuza uchumi hivyo kujengwa kwa miundombinu ya
masoko, vivuko vya madaraja, barabara na miundombinu ya huduma za kijamii kutawezesha
kutoka katika biashara za kijadi kwenda katika biashara ya kimataifa na hivyo
kukuza uchumi na kipato cha wananchi wa Mkoa wa Kigoma.
Soko la Kimataifa
lililopo Wilayani Buhigwe katika Kijiji cha Nyamgali
|
Mahindi yaliyo
hifadhiwa kienyeji Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma, Mkoa wa Kigoma upo katika
orodha ya Mikoa ya uzalishaji hapa Tanzani.
|
Bidhaa
mbalmbali zitokanazo mazao ya nyuki Mkoani Kigoma, mbali na kuuza asali
wananchi hutengeneza bidhaa kama mishumaa na kuongeza kipato.
|
Soka la Kimataifa
lililopo Wilayani Buhigwe katika Kijiji cha Nyamgali
|
Mazao kama vile muhogo,
karanga, ulezi inasemekana ndiyo chakula kitumiwacho na wakazi wa Burundi na
kongo, mkoa wa Kigoma unazalisha mazao ya aina zote kwa hakika masoko ya mazo
haitakuwa shida tukiwa na Miundombinu ya uhakika.
Aidha ujenzi wa bandari
kavu katika eneo la Katosho Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni faraja kubwa kwa
wafanyabishara kutoka nchini Burundi ambao wamekuwa wakitoa maombi yao kwa
uongozi wa Mkoa waruhusiwe kupitisha mizigo yao kupitia Barabara ya Dar es
Salaam Nyakanazi- Kibondo- Kasulu kutoka bandari ya Dar es Salaam, badala ya Dar es salamm-Nyakanazi- Rusahunga ambayo ni
ndefu na ni gharama kubwa kwao.
Kwa hakika Miundombinu
hususan ya Mawasiliano katika Mkoa wa Kigoma imeimarika, jitihada na nguvu ya
Serikali zinaonekana wazi kwa wananchi, waswahili husema “ndondondo si chururu”
miaka michache mambo yote yatakamilika kwani hatani mji wa Roma haukujengwa kwa
siku moja.
Habari zote na Picha- Afisa Habari wa RS Kigoma
No comments:
Post a Comment