Zaidi ya silaha haramu 5600 zimeteketezwa moto Mkoani Kigoma ikiwa ni moja ya hatua za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa silaha haramu nchini.
Akiongoza
zoezi la uteketezaji wa silaha hizo Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Ndani ya Nchi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba alisema “tatizo la
uzagaaji wa silaha ni la kidunia, kwa kiwango kikubwa uzagaaji wa silaha hovyo
umeathiri maendeleo kiuchumi, kisiasa na Kijamii”
Aidha
ameongeza kuwa tangu Januari 2017, amefuta ukimbizi wa Makundi kama ilivyokuwa
awali na utaratibu utakuwa kila Mkimbizi ataingia nchini baada ya kuhojiwa na
kujadiliwa na Kamati husika.
Alitoa
rai kwa Watazania wote wanaomiliki Silaha kinyume na taratibu za nchi
kuzisajili au kuzisalimisa silaha hizo, na mwisho wa zoezi hilo itakuwa tarehe
30 Juni, 2017, baada ya hapo hatua kali za watakaobainika zitachukuliwa.
Silaha
zilizoteketezwa zilikamatwa kutoka katika Mikoa ya Mara, Mwanza, Simiyu,
Shinyanga, Tabora, Katavi, Rukwa, Kagera na Kigoma.
Hata
hivyo Mkoa wa Kigoma umetajwa kuongoza kwa uzagaaji wa Silaha haramu kwa
asilimia zaidi ya 40% na matukio
yanayohusisha silaha kwa 20 % ukiligaishwa na Mikoa Mingine.
Akizungumza
katika zoezi la Uteketezaji wa Silaha hizo Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo
Nsato Marijani Msanzya alisema Mkoa wa Kigoma unaogoza kutokana na kupakana na
nchi zenye machafuko ya Kisiasa, kupokea wakimbizi wengi ambao huingia kwa makundi bila kupekuliwa,
baadhi yawakimbizi wasio waaminifu hutumia mwanya wa ukimbizi vibaya kwa kufanya
matendo mengi ya kihalifu.
Hadi
sasa wakimbizi waliopo Mkoani Kigoma ni zaidi ya 27,000 ambao ni chimbuko la
uzagaaji wa silaha haramu Mkoani Kigoma. Imeelezwa kuwa katika Mkoa wa Kigoma
kwa siku hupokea wakimbizi 400 hadi 500 wakitokea Nchi jirani za Burundi na
Congo.
Hata
hivyo taarifa zinasema wengi wao sasa
hawakimbi kwa hofu ya machafuko ya kisiasa bali wanakimbia njaa na ugumu wa
maisha nchini mwao.
Naye
Naibu Kamishna wa Polisi Sekretarieti ya Umoja wa Kikanda wa Kushughuliikia
uzagaaji wa silaha Bw. Theonest Mshindashaka alisema Jumla ya Silaha
zilizokwisha kuteketezwa kati ya 2014 hadi 2017 ni zaidi ya 17,000.
Uteketezaji
wa silaha haramu umefadhiliwa na Serikali ya Marekani Kitengo cha Kupambana na
Uzagaaji wa Silaha.
Silaha mbalimba za moto zipatazo 5608 zikiwa zimeandaliwa tayari kwa Kuteketezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma |
Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (MB) akiwasha moto Silaha haramu kupitia Mfumo maalumu wa ulipuaji |
Habari zote na
G.D. Ng'honoli
G.D. Ng'honoli
Afisa Habari na Mawasiliano wa Sekretarieti ya Mkoa wa
Kigoma
No comments:
Post a Comment