Tuesday 19 December 2023

UJENZI SHULE YA MSINGI MAHAHA KUWAONDOLEA ADHA WANAFUNZI KUTEMBEA KM 20

Ujenzi wa Shule ya Msingi Mahaha  umetajwa kuwaondolea adha ya kutembea zaidi ya Km. 20 wanafunzi kutoka Kitongoji cha Mahaha kilichopo kijiji cha Magalama Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma. Baadhi ya wakazi katika kitongoji hicho wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwasogezea huduma hiyojirani kwani itaimarisha Usalama wa watoto wao kwenda na kurejea kutoka shule.

"Watoto wengi walikuwa watoro, wengine waliacha shule na hata baadhi ya wazazi kuhofia kuwaandikisha watoto Elimu awali na Msingi kutokana watoto hao kutomudu kutembea umbali huo pamoja na kuhofia  usalama wao wakiwa njiani kwani kuna nyakati hurejea nyumbani usiku au hunyeshewa na mvua" ameeleza Theresia Kanwa.

Akitoa Taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Afisa Elimu Awali na Msingi Oliver Mgeni amesema Miundombinu imekamilika na kuanzia Januari 2024 itapokea wanafunzi  wa Elimu Awali na Msingi kuanzia Darasa la kwanza hadi la Saba.

Tunaishukuru serikali kupitia mradi wa BOOST kwa kutenga fedha kiasi cha Shilingi 361,500,000 ili kujenga Shule hii kwani watoto wote kutoka kitongoji cha Mahaha waliokuwa wakisoma katika kijiji cha Magalama watarejeshwa hapa ili wasome katika shule hii ya kisasa iliyojengwa jirani na makazi yao" amesema Oliver Mgeni kupitia taarifa hiyo

Baadhi ya wakazi katika kitongoji hicho wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwasogezea huduma hiyojirani kwani itaimarisha Usalama wa watoto wao kwenda na kurejea kutoka shule.

"Watoto wengi walikuwa watoro, wengine waliacha shule na hata baadhi ya wazazi kuhofia kuwaandikisha watoto Elimu awali na Msingi kutokana watoto hao kutomudu kutembea umbali huo pamoja na kuhofia  usalama wao wakiwa njiani kwani kuna nyakati hurejea nyumbani usiku au hunyeshewa na mvua" ameeleza Theresia Kanwa.

No comments:

Post a Comment