Matumizi
ya Simbomilia (Barcordes) au alama za utambuzi wa bidhaa katika masoko ni jambo
lisilokwepeka kwa sasa ambapo Tanzania inaelelekea kweye nchi ya uchumi wa kati
na viwada.
Haya yameelezwa na Mkurugezi wa Taasisi ya Global Standard one (GS1)
Tanzania Bi. Fatma Kange Salehe wakati wa kutia saini ya makubaliano na
Halmashauri nane za Mkoa wa Kigoma.
Mkataba
wa Makubaliano na Taasisi ya GS1 Tanzania unalenga kuwapa mafunzo na kuwajengea
uwezo wajasiriamali katika Halmashauri ili waweze kutambua umuhimu wa kuwa na alama
za utambuzi wa bidhaa katika masoko wanazozizalisha.
Mafunzo
hayo yanatarajiwa kuzijumuisha Taasisi mbalimbali zitakazoshiriki katika utoaji
wa mafuzo hayo kwa wajasiriamali kama vile Wakala la Vipimo, Mamlaka ya Mapato
Tazania, Shirika la Viwago Tanzania, BRELLA, SIDO, TANTRADE.
Matarajio
baada ya mafunzo haya ni, kuongezeka kwa mapato ndani ya Halmashauri, bidhaa
nyingi kuwa katika soko rasmi kitaifa na kimataifa, kuongeza mnyororo wa
thamani ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali, kuongezeka kwa wajasiliamali
katika Halmashauri na, kuwanyanyua kiuchumi wajasiliamali wadogo.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (mst) ambaye
alishuhudia utiwaji wa makubaliano hayo kati ya GS1 Tanzania na Halmashauri za
Mkoa wa Kigoma alisema kuwa lengo la Serikali ya Mkoa wa Kigoma ni kuhakikisha
kwamba fursa zote za kilimo, uvuvi na madini zinafanyiwa kazi kisasa zaidi ili
wananchi waweze kumiliki Uchumi. “ili wananchi wetu waweze kunufaika na kilimo,
vuvi, madini lazima kuwepo na mbinu
sahihi za kuongeza thamani kwenye bidhaa zao wanazozalisha na zikubalike katika
masoko ya ndani nje” alisisitiza.
“Ninaamini
makubaliano haya yatakuwa na matokeo chanya ambayo yatawezesha bidhaa nyingi za
Tanzania hususani wananchi wa Kigoma kuingia katika Masoko ya ndani na nje ya
nchi hivyo kuinua pato la mtu mmoja mmoja na hatimae taifa zima” aliongeza
Maganga.
Aidha,
amewaasa watanzania kuanza kutumia Simbomilia (barcordes) za Tanzania badala ya
kutumia za nje ya nchi. Alisisitiza kuwa kutumia simbomilia za Tanzania
kutapunguza matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kulipia uduma hiyo,
pia itasaidia kutoa takwimu rasmi za wazalishaji wa Kitanzania, kwani
unapotumia simbomilia za nje ya nchi bidhaa huonekana imetoka nchi nyingine na
siyo Tanzania hata kama imezalishwa hapa nchini.
Kutokana
na umuhimu wa jambo hili Maganga amewaagiza Wakurugenzi kuanza mafunzo haya kwa
wajasiliamali ndani ya Miezi miwii tangu kutiwa saini ya Makubaliano na Taasisi
ya GS1 Tanzania.
No comments:
Post a Comment