Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Pallangyo akifungua warsha ya kuandaa mpango kazi wa motisha na vivutio kwa watumishi |
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Pallangyo amefungua warsha ya siku sita yenye
lengo la kuzijengea uwezo Halmashauri za Mkoa wa Kigoma kuandaa mpango kazi
wenye lengo la kutoa motisha na vivutio kwa watumishi ili waweze kubaki katika
maeneo ya vituo vya kazi wanapopangiwa.
Amesema
maeneo yaliyopo pembezoni ambako huduma za kijamii, kiuchumi na miundombinu
bado havijaimarika na hivyo kuwa changamoto kwa watumishi wanapopangiwa kazi
katika maeneo hayo.
Akiwashukuru
wafadhili wa mafunzo hayo Shirika la Marekani USAID kupitia PS3, amesema warsha hiyo itasaidia serikali za
mitaa kuwa na uwezo sio tu wa kuwabakisha watumishi wanapopangiwa kufanya kazi
bali pia kuinua kiwango cha ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.
“Nataka
niwaeleze viongozi wa halmashauri mnapaswa kusimamia zoezi hili ili liwe
endelevu tukifanya kazi yetu vizuri, wafanyakazi ari ya kufanya kazi pia
kupunguza idadi ya wafanyakazi kutokaa maeneo ya kazi pindi wanapopangiwa alisema”
Pallangyo.
Naye
Afisa Sera na uraghabishi wa shirika la PS3 Christina Godfrey, amsema wameamua
kutoa mafunzo haya baada ya kufanya utafiti kwa halmashauri 33nchini Tanzania
ambapo katika maeneo yenye changamoto Kigoma nayo ilionekana kuwa miongoni. PS3
imeona kuna umuhimu wa kutengeneza mazingira rafiki ya kikazi kwa kuwafundisha
watendaji katika Halmashauri kuwa na mipango mkakati ya kutoa motisha kwa
wafanyakazi.
Warsha
hiyo imehudhuriwa na Maafisa Utumishi, Maafisa Elimu na Makatibu wa Hospitali
kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Kigoma.
No comments:
Post a Comment