Sunday 17 December 2023

UKIHUJUMU MIUNDOMBINU YA UMMA HUMKOMOI KIONGOZI

Wanafunzi wa shule za msingi kutoka vitongoji vya NYAKASERO,  MURUGABA na MKUYUNI katika kijiji cha NYAMTUKUZA wilayani KAKONKO Mkoani KIGOMA wameondokana na adha ya kutembea umbali wa zaid ya kilomita kumi kwa miguu kufuata elimu katika shule ya msingi Nyamtukuza.

Kero hiyo imeondoka baada ya serikali kutoa Zaid ya shilingi milioni 360 kupitia mradi wa Boost kwajili ya ujenzi wa shule mpya ya mfano yenye viwango vya kimataifa ambayo tayari imekamilika kwa asilimia mia moja.

Shule hiyo yenye michoro, Bembeya na maeneo ya michezo kwaajili ya watoto wadogo inatajwa kuwa moja ya shule chache za msingi zenye viwango vya kimataifa zilizopo mkoani Kigoma na kutarajiwa kuanza kutumika januari mwakani.

Mkuu w mkoa wa kigoma Thobias Andengenye akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi wa kwanza wa kulinda miundoimbinu ya umma waliojengewa na serikali ili iweze kuwahudumia kwa muda mrefu

Andengeye akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Murugamba na Nyakasero na kusisitiza kuwa serikali haitawafumbia macho watu watakao bainika kuihujumu miundombinu ya serikali na kama wenyeji wa maeneo  hayo wakifumbia macho na kutotoa taarifa ya ubadhirifu au wizi wa aina yoyote katika miundombinu inayowahudumia itawasababishia watoto wao kukosa huduma muhimu karibu na maeo yao

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko MHULI NDAKI akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Kigoma kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya mfano na kusema licha ya mradi huo kutokuwa na gharama za ununuzi wa samani lakini ofisi yake imeshaweka utaratibu wa kuhakikisha shule hiyo inakuwa na samani za kisasa zenye hadhi sawa na majengo hayo

No comments:

Post a Comment