Tuesday 19 December 2023

MSIWAANGAMIZE WATOTO WENU

 Mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye ametoa wito kwa wananchi wa jamii ya wafugaji na wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini kutumia fursa ya uwepo wa miundimbinu bora ya elimu inayojengwa na serikali kuwasomesha watoto wao

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza na wananchi wa kata ya Nyamtukuza wilayani Kakonko na kusema elimu ndio dira itakayomsaidia mtoto kuyamudu mazingira anayoishi na kuacha kuwasomesha watoto ni kuaangamiza mustakabali wao maisha yao katika siku za usoni. 

KAULI YA Andengenye imekuja kufuatia serikali kujenga shule ya sekondari katika kitongoji cha LUTENGA katika wilaya ya KAKONKO mahali ambapo wengi wanaoishi hapo ni wafugaji na wachimbaji wa madini waliohamia miaka ya hivi karibuni.

Wakazi wa Lutenga kata Nyamtukuza wilayani Kakonko wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kigoma mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari katika kitongoji hicho.
Mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondri katika kitongoji cha Lutenga

Wanafunzi wa maeneo hayo walikuwa wakisumbuka kutembea umbali wa zaid ya kilomita thelathini kufuata elimu ya sekondari katika kijiji cha Nyamtukuza na kusababisha wengine kukatiza masomo kwa kushindwa kumudu adha hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kakonko MHULI NDAKI akitoa taarifa ya ujenzi wa shule ya sekondari katika kitongoji cha Lutenga na kusema serikali imetoa jumala ya shilingi Bilioni moja na milioni mia mbili kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya, shule na soko katika kata ya nyamtukuza na utekelezaji wa miradi yote hiyo upo zaid ya asilimia tisini na kutarajiwa kukamilika mapema mwezi ujao

Kwa upande wao wananchi wa kata hiyo wameishukuru serikali kwa ujenzi wa miradi ya maendeleo katika eneo lao na kuwaondolea adha ya kusafiri kwenda wilaya Biharamulo mkoani Kagera kufuata huduma mbalimba za kijamii ilihali kiutawala wapo wilaya ya kakonko mkoani Kigoma

No comments:

Post a Comment