Thursday 18 April 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Gen. (Mst.) Emmanuel Maganga leo amekutana na Bw. Vincent Rico Mkuu wa Mradi wa Madaktari wasio na Mipaka na kuzungumzia namna ya kuendelea kuboresha huduma za Afya Mkoani Kigoma.
Bw. Rico ameeleza kuwa Medical Sans Frontiers (MSF) wataendelea kutoa misaada mbalimbali katika sekta ya afya ikiwemo kusaidia kupambana na Malari, kuangalia namna ya kusaida madawa pamoja na vitendea kazi katia Hospitali na vituo vya Afya Mkoani Kigoma.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ametoa shukrani kwa MSF kwa juhudi zao kubwa katika kuusaidia Mkoa wa Kigoma kwenyemasuala ya sekata ya Afya, amesisitiza kuwa Mkoa wa Kigoma utaendelea kutoa ushirikiano wakati wote ili kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Kigoma wanapata huduma bora za afya. 




No comments:

Post a Comment