Picha ya majengo ya Utawala na Madarasa yatakavyokuwa baada ya ujenzi Kigoma Grand high School kukamilika |
Pichan ya jengo ya Bwalo litakavyokuwa baada ya kukamilika ujenzi Kigoma Grand high School kukamilika |
Eneo la majengo ya mabweni yatakavyokuwa baada ya ujenzi Kigoma Grand high School kukamilika |
Kigoma
yaanza kutekeleza mpango wa “Matokeo Makubwa Sasa” katika Sekta ya Elimu
Ili kuimarisha na kuboresha elimu ya Msingi na Sekondari mkoa
umeweka mipango na mikakati mbalimbali kuhakikisha inatimiza adhima ya Serikali
ya mpango wa Matokeo Makubwa sasa.
Katika kukabiliana
na upungufu wa shule za kidato cha tano na sita Mkoa umeanzisha mradi wa shule Kuu ya Mkoa
itakayoitwa (Kigoma Grand High School) itakayogharimu jumla
ya Tshs. 29 bilioni, fedha hizi zitatumika kujenga madarasa,
maabara, nyumba za walimu, huduma za jamii (maji, umeme, afya), maktaba, bwalo
samani, majengo ya utawala, uzio wa shule, viwanja vya michezo na miundombinu
mingine. Mchakato wa kupata fedha kwa jili ya ujenzi ulikwishaanza, hadi sasa michango
imefikia kiasi cha Tshs. 237,041, 700.00
Kigoma
Grand Kigh School inatarajiwa kuwa na michepuo ya masomo ya Sayansi 9 na Sanaa
5 ambapo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi kuanzia 1120 wasichana na
wavulana.
Mkoa umedhamiria kuongeza
ufaulu wa mitihani ya Taifa ya darasa la saba kutoka 31% na Mitihani ya Kidato
cha nne kutoka 43% kufikia 60% mwaka 2013. Aidha katika kuinua ufaulu mafunzo ya ziada kwa walimu wa
shule za msingi wanaofundisha masomo ya Sayansi na Hisabati kutoka shule 206
hadi sasa yametolewa kwa walimu 412, hata hivyo mpango huu unategemewa kufanyika
hadi ngazi ya walimu wa shule za sekondari.
Mipango mingine ni pamoja na kuongeza
idadi ya uandikishaji wanafunzi wa awali na darasa la I, Kuhakikisha kuwa
wanafunzi wa darasa la II wanajua KKK Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kabla ya
kuingia darasa la III, Mkoa unashirikisha wazazi na wadau wa elimu katika
ujenzi wa miundombinu inayopungua katika shule zilizo katika kila halmashauri.
Mkoa unaishukuru serikali ya
awamu ya nne kwakuupa Mkoa wa Kigoma kipaumbele wa kipekee na wa makusudi
kabisa hasa katika kuimarisha miundombinu ya barabara kama ile ya Kidahwe –
Nyakanazi; Kasulu – Uvinza – Katavi na Kidahwe – Ilunde – Tabora. Hali hii itavutia
watu wengi kuja na hasa wafanyakazi wa sekta mbalimbali kufanya kazi katika
Mkoa huu tofauti na hapo awali hivyo itachochea maendeleo na kuvutia wawekezaji
na uwekezaji ndani ya mkoa wetu wa Kigoma.
Safi sana, ila mpango usiishie kwenye makaratasi tu.
ReplyDelete