Monday 23 December 2013

DASIP yakamilisha Miradi ya Kilimo 294 Katika Mkoa wa Kigoma



Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali (Mst.) Mhe. Issa Salehe Machibya akihutumia washiriki wa warsha ya wadau wa Uendelezaji wa Mazao ya Kilimo (hawapo pichani) iliyofanyika leo Mkoani Kigoma, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe, Athuman Maneno na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Peter Killewo.
Mhe. David Kafulila Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini akichangia hoja katika warsha ya wadau wa uendelezaji wa mazao ya Kilimo iliyofanyika leo Mkoani Kigoma mapema
wenye viti wa Halmashauri za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko na Uvinza wakifuatilia kwa makini makablasha yenye mada mbalimbali kagika warsha ya wadau wa uendelezaji wa mazao ya kilimo iiyofanyika leo Mkoani Kigoma
Washiriki wa Warsha wakiwa katika picha ya Pamoja muda mfupi baada ya warsha hiyo kufunguliwa.
DASIP yakamilisha Miradi ya Kilimo 294 Katika Mkoa wa Kigoma
Jumla ya miradi ya Kilimo 294 ikiwemo miradi ya miundombinu ya kilimo 140, na miradi ya teknolojia za kilimo 154  imetekelezwa katika Mkoa wa Kigoma na Mradi wa Uwekezaji Katika Sekta ya Kilimo (District Agriculture Sector Investment Project (DASIP). Kwa kipindi cha miaka saba (7)

miradi ya miundombinu ya kilimo iliyotekelezwa na DASIP katika Mkoa wa Kigoma ni pamoja na Majosho , Machinji, Malambo na Visima vifupi vya maji, Masoko na Maghala na Barabara. Aidha kwa upande wa miradi ya teknolojia za kilimo ni utoaji wa Matrekata ya mkono, mashine za kusaga nafaka, mashine za kusindika maziwa, mashine za kukoboa na kushakata azao mbalimbali, na mashine za kusukuma maji na vifaa vya kukokotwa na wanyama kazi.
Haya yameelezwa katika leo naAfisa Tathmini na Ufuatiliaji wa DASIP  Bw. Israel Mwakilasa katika warsha ya wadau wa uendelezaji wa mazo ya Kilimo iliyofanyika Mkani Kigoma kwa kuwaktanisha viongozi wa serikali, Taasisi, sekta binafsi na Asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.
Bw. Mwakilasa amesema malengo makuu ya DASIP ni kumfanya mkulima na mfugaji alime kwa tija  na  uhakika wa kupata mazao yenye ubora na uhakika wa masoko.
Akichangia katika warsha hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali (Mst.) Mhe. Issa Salehe Machibya amewataka Wakurugenzi Kuweka vipaumbele katika bajeti zao ili kuwawezesha wakulima na vikundi vya wakulima kujenga miradi mbalimbali ya kilimo, Mkoa wa Kigoma kwa sas umeomba kuwekwa katika Mikoa ya Uzalishaji chakula kama ilivyo mikoa ya nyanda za juu kusini kwani unazo fursa nyingi za kuufanya uzalishe chakula kwa wingi.

1 comment:

  1. Wakulima waelimishwe zaidi na kupatiwa fursa za kupata mikopo ya kutosha kufanya kilimo cha kibiashara.

    ReplyDelete