Tuesday, 24 December 2013

Mkataba wa Huduma kwa Mteja Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma kuanzishwa Mwakani 2014


Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Serikali za Mitaa Bw. Moses Daniel Msuluzya akitoa maada mbele ya Maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya Maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma wakifuatilia mada katika kikao cha Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma.

Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma imeshauriwa kuandaa na Kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Chatter)  ili kuleta ufanisi katika kutoa huduma  bora na kwa Wakati  kuendana na mpango wa Matokeo Mkaubwa sasa.
Haya yameelezwa na Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Serikali za Mitaa Bw. Moses Daniel Msuluzya Wakati akitoa mada ya Mahusiano ya Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Kikao cha Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma  cha kujadili Maoteo  ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2014/2015 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma.
Bw. Msuluzya alisema Mkataba wa Huduma kwa Mteja utasaidia kufanya kazi kwa matokeo ya haraka na kumwezesha mtumishi kupimwa kadiri ya utendaji wa kazi itasaidia vilevile mtumishi afanye kazi kwa tija lazima kuwepo na Mpango amhsusi unaomfanya atambu kuwa anapaswa kufanya nini na kwa muda gani, kuondoa dhana ya utendaji wa mazoea.


Kumekuwa na tatizo la kutatoa Taarifa kwa Wakati kwa baadhi ya sekta jambo ambalo linasababishwa na kasoro za kiutendaji na kutokuwa na Mkataba wa Huduma kwa Mteja, ili kuondoa tatizo hii lazima uwepo mpango wa Kuzindua Mkataba wa huduma kwa Mteja ili uanze kufanya kazi haraka.
Aidha aliongeza kuwepo na Uimarishwaji wa kupashana habari kati ya Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Tovuti, Blogu za Halmashauri na Mkoa ili kusaidia katika kuimarisha mahusiano ya karibu ya watendaji wa Halmashaur na Mkoa na hivyo kurahisisha utendaji kazi kwa ufanisi wa hali ya juu pamoja na kufahmu nini kinaendelea kwa pande zote mbili. 

Akihitimisha kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi Peter Killewo amewataka watendaji wa Sekretariei ya Mkoa wa Kigoma kuanza kufanya mchakaato wa kuandika  mpango wa Hudua kwa Mteja ili kufikia Januari mwakani 2014 uweze kukamilika.

No comments:

Post a Comment