Friday, 13 December 2013

Taasisi ya Jane Goodall yaendelea kushirikiana na Mkoa wa Kigoma katika kuhifadhi Mazingira.

Bi. Jane Goodall akielezea namna taasisi yake inavyoendelea kutoa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kuwalinda Sokwe waliopo katika hofadhi ya Taifa ya Gombe Mkoani Kigoma, pembeni yake ni wajumbe alioambatana nao alimpomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma hivi karibuni

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Mhe. Lt. Col (Mst) Issa Salehe Machibya akifuatilia jambo kwa muwasilisha mada (hayupo pichani) ya namna Mkoa wa Kigoma unavyochukua jitihada za Makusudi katika kulinda na kuhifadhi mazingira, kushot ni baadhi ya maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma na Wajumbe walioambatana na Bi. Jane Goodall.

Bi Jane Goodall akiwa na mdoli akieleza namna anavyopenda kuishi na kufahamu maisha ya mnyama sokwe.

Afisa Maliasili na Misitu wa Mkoa wa Kigoma Bw. Cheyo Kashinje Mayuma akielezea mbele ya Bi. Jane Goodall na wajumbe wengine mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli za kuhifadhi na kulinda mazingira Mkoani Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Lt. Col (Mst) Issa Salehe Machibya akitoa Maelezo ya picha ya mti wa aina ya Miombo kwa Mwanzilishi wa Taasisi ya Jane Goodall.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Lt. Col (Mst) Issa Salehe Machibya akimkabidhi zawadi ya picha ya mti wa aina ya Miombo Bi. Jane Goodall ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya Jane Goodall  inayojishughulisha na utafiti wa Sokwe katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe, sambamba na utafiti huo taasisi hii hujihusisha na uhifadhi wa mazingira Mkoani Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Lt. Col (Mst) Issa Salehe Machibya akimkabidhi zawadi ya kinyago cha Sokwe Bi. Jane Goodall ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya Jane Goodall  inayojishughulisha na utafiti wa maisha ya wanyama aina ya Sokwe katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe, sambamba na utafiti huo taasisi hii hujihusisha na uhifadhi wa mazingira Mkoani Kigoma.

No comments:

Post a Comment