Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Lt. Col (Mst) Issa Salehe
Machibya akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2013 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mhe. Peter
Kiroya muda mfupi baada ya kuupokea kutoka Mkoa wa Kagera.
|
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma /Ujiji Mhandisi
Christopher Nyambele akicheza kwa furaha Wakati Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 zilipowasili
katika Manispaa yake.
|
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2013, Mhe. Juma
Ali Simai akifungua rasmi Stenndi ya Mabasi ya Mkoa wa Kigoma iliyopo eneo la
Mwasenga katika Manipaa ya Kigoma /Ujiji.
|
Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013 zilihitimishwa
katika Mkoa wa Iringa tarehe 14 Ocktoba 2013, ambapo Wilaya ya Kakonko Mkoani
Kigoma imejipatia zawadi ya shilingi 10,000,000 baadaya kuibuka mshindi wa
kwanza katika mbio za mwenge wa uhuru
mwaka 2013.
Akitangaza katika kilele cha mbio za mwenge wa
uhuru 2013, Waziri wa Habari Utamaduni na michezo Mhe. Fenera Mkangara alieleza
kila mwaka Mwenge wa Uhuru huzingatia vigezo vinavyopangwa kwa mwaka husika, na
vigezo hivyo hushindanishwa kwa kila Mikoa,Wilaya na Halmashauri. Mwaka 2013
wilaya iliyofanya vizuri na kuibuka mshindi dhidi ya wilaya zote hapa Tanzania
bara na Viziwani ni Wilaya ya Kakonko.
Wilaya ya kakonko ni mojawapo ya Wilaya tatu mpya
zilizoanzishwa mwaka huu Wilaya ya Kakonko ikizaliwa na Wilaya mama ya Kibondo,
sababu za Msingi zilizoifanya Wilaya hii kuibuka mshindi pamoja na uchanga wake
ni kuwa na miradi bora iliyokamilika na inayowalenga wanchi moja kwa moja.
Baadhi ya miradi iliyozinduliwa na kuwekewa mawe
ya Msingi katika Wilaya ya Kakonko ni pamoja na umeme, maji, afya na elimu.
Mbio za mwenge wa uhuru zimekuwa kichocheo kikubwa kwa nchi katika kuhamasisha
maendeleo mbalimbali ambapo miradi mingi imekamilishwa kwa nguvu za wananchi
kuchangia fedha au nguvu kazi.
Sambaba na kuhamasisha manendeleo ya wananchi
mwenge wa uhuru umeendeleza umoja, amani mshikamano wa watanzania.
Karibuni kaika blgo hii kupata habari mbalimbali za Mkoa wa Kigoma, Fursa za uwekezaji
ReplyDelete