Thursday, 12 December 2013

Ziara ya Waziri Mkuu yaelezea Maendeleo na Matumaini kwa wananchi wa Kigoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akiteremka katika Uwanja Ndege wa Kigoma kwa ziara ya kikazi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali (Mst) Issa Salehe Machibya akiteta jambo na Mhe. Waziri Mkuu mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2013 .
Mhe. Waziri Mkuu wakiwa na Mkewe mama Tunu Pinda wakipata burudani  ya ukaribisho kutoka kikundi cha ngoma cha Mapigo Saba katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2013 . .
Mhe. Waziri Mkuu akisalimiana na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2013 . .
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akimweleza jambo mgeni wake Waziri Mkuu mara baadaya ya kusalimiana na wananchi wa Mkoa wa Kigoma mapema mwezi Oktoba 2013.
Waziri Mkuu na Ujembe alioambatana nao katika ziara yake wakisikiliza taarifa ya silaha mbalimbali zilizokamatwa mwaka 2012/2013 hadi kipindi cha zoezi la kuwaondoa nchini wahamiaji haramu (Operation Kimbunga).
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Fraizer Kashai akimwonesha Waziri Mkuu aina za Silaha zilizo kamatwa kwa kipindi cha mwaka 2012 na 2013.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Fraizer Kashai akimwonesha Waziri Mkuu aina za risasi zilizo kamatwa kwa katika zoezi la kuwaondoa nchini wahamiaji haramu (Operation Kimbunga).
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Issa S. Machibya akimwonesha moja ya ganda la risasi Mhe. Waziri Mkuu

Waziri Mkuu akikagua bidhaa mbalimbali zitokanazo na mazao ya nyuki wasiouma katika Kijiji cha Itumbiko Wilayani Kakonko alipofanya ziara yake mwezi wa Oktoba 2013.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia(MB) akikagua Asali ya nyuki wasiouma Wilayani Kakonko wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda mwezi Oktoba 2013.

Mhe. Philipo Mlugo akifafanua jambo juu ya Sekta ya Elimu  kwa wanchi wa Wilaya ya Kakonko (hawapo pichani) katika ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani mwezi Oktoba 2013





Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu walipotembelea hifadhi ya msitu wa kijiji cha  Nduta Wilayani Kibondo.
Mtaalamu wa Nyuki katika Wilaya ya Kibondo akielezea kwa Waziri \Mkuu namna ya kuzalisha malkia wa nyuki na vifaa vinavyotumika.


Waziri mkuu akapatiwa nafasi ya Kutundika mzinga mmoja wa nyuki kama ishara ya Kuzindua mradi na Kuweka Baraka zake katika mradi huo

Waziri Mkuu akipata maelezo ya namna ya utengenezaji wa Mizinga ya nyuki na namna ya kutundika mizinga hiyo.

Mhe. Mizengo Pinda akisisitiza utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika Bwala la Maji lililojengwa hivi karibuni katika kijiji cha Twabagondozi Wilayani Uvinza.

Wananchi Wilayani Kibondo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Pinda (hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo mwezi Oktoba, 2013.

Waziri Mkuu akifafanua jambo kwa wananchi Wilayani Kibondo wakati alipowahutubia mwezi Oktoba, 20013.

Soko la Mpakani (mwonekano wa ndani) lililopo katika Kijiji cha Nyamgalili Wilayani Buigwe lilizinduliwa na Mhe. Mizengo Pinda

Soko la Mpakani (mwonekano wa nje) lililopo katika Kijiji cha Nyamgalili Wilayani Buigwe lilizinduliwa na Mhe. Mizengo Pinda



Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akipata burudani kutoka katika kikundi cha ngoma cha Warumba asilia muda mfupi kabla ya kuwaaga wananchi wa Kigoma.
Picha zote na G.D. Ng'honoli- Afisa Habari wa RS Kigoma



Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB) aliyoifanya katika Mkoa wa Kigoma kuanzia tarehe 01 Octoba, 2013 hadi 06 Octoba, 2013. Katika ziara yake Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliambatana na Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbalimbali.
Mhe. Waziri Mkuu ametembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo na Umwagiliaji, elimu, Maji na Afya, vilevile miradi ya miundombinu ya Barabara, biashara na masoko.
Katika ziara hiyo mhe. Mizengo aliahidi kuvisaidia vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na ufugaji wa nyuki na kilimo cha zao la mhogo. Aidha aliwaeleza na kuwasisitiza wakurugenzi na viongozi mbalimbali wa Mkoa kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia zaidi wakulima ili walime kitaalamu.
Alisema hatapenda kuona viongozi wasioibua mawazo ya kubuni miradi ya maendeleo kwa wananchi wao “ baadhi ya viongozi wanakaa ofisini tu ukiwauliza wananchi umewasaidiaje kufanya shughuli za maendeleo, kiongozi usisubiri wananchi wewe ndiyo unatakiwa uwaongoze kuona mbali alisema Waziri Mkuu
Suala la kuwaondoa nchini wahamiaji haramu amelisisitizia kuwa litakuwa endelevu, wananchi watoe ushirikiano kwani linalenga kudumisha amani na usalama wa nchi.
Sambamba na zoezi la kuwaondoa nchini wahamiaji haramu alitoa angalizo pia kwa migogoro ya wakulima na wafugaji inayoanza kuibuka katika mkoa wa Kigoma akisema kuwa wafugaji waliopo mkoani Kigoma ni wa aina mbili yaani wafugaji kutoka mikoa iliyomo ndani ya nchi hasa kanda ya ziwa na wafugaji kutoka nchi jirani.
Mhe. Waziri alisema wafugaji kutoka nje ya nchi waondolewe mara moja bila mjadala, kwa wale watanzania ameuagiza mkoa uone namna ya kugeuza wafugaji hao kuwa fursa badala ya kuwafukuza kwani utaratibu utengenezwe kati ya mikoa wanakotoka na wanakotaka kuhamia ili wapatiwe maeneo kwa uhalali kuliko wanavyofanya kwa sasa bila kufuata sheria.
Mhe. Pinda amesema serikali ya awamu ya nne inayo nia ya dhati ya kuuendeleza mkoa wa Kigoma katika Nyanja mbaloimbali, akiwa ameambatana na baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliweza kutoa ufafanuzi juu ya masuala na mipango ya wizara zaao kuhusu mkoa wa Kigoama
Katika miundombinu ya Barabara Waziri Mkuu aliwaambia wananchi kuwa miradi iliyopewa kipaumbele katika mkoa wa Kigoma kwa sasa ni ule mrdi wa Barabara ya kidahwe hadi Tabora ambayo ipo katika hatua za kukamilishwa kujengwa, vilevile Barabara ya Kidahwe hadi Nyakanazi ambayoimetengewa fedha kiasi cha shilingi bilioni---ambazo zitakamilisha km 20 za mwanzo .
Umeme na maji serikali inaendele kukamilisha miradi mikubwa kila Wilaya ya maji na  umeme, matahalani kwa sasa inasambaza umeme vijijini kupitia kampuni ya REA ambapo karibu vijiji 10  kila Wilaya vitapata umeme kwa awamu ya kwanza, hata hivyo mradi wa kupata umeme kupitia Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma hadi Nyakanazi unaaandaliwa ili kuwapa wananchi wa Kigoma umeme wa Gridi ya Taifa. Aliwaomba wananchi waendelee kuiamini serikali na kushirikiana nayo kwa utulivu na amani.

No comments:

Post a Comment