Wakuu wa Wilaya na Watendaji
Katika Halmashauri watakiwa kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.
Luteni Kanali (Mst) Issa Salehe Machibya amewaagiza Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa
Kigoma pamoja na Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanashughulikia migogoro
kati ya wakulima na wafugaji inayojitokeza katika maeneno yao kwa haraka ili
kuepusha majanga makubwa yanayoweza kusababishwa na migogoro ya aina hiyo.
Kanali machibya ametoa maagizo
hayo mapema wiki hii Wakati akihitimisha kikao cha dharura cha Kamati ya
Ushauri ya Mkoa kilichofanyika katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma,
kikao hicho kiliitishwa kwa nia ya kupokea na kujadili Taarifa za ugawaji wa
maeneo mapya ya Kiutawala yaliyoongezeka katika Halmashauri na Manispaa ikiwemo
Vijiji, Vitongoji, Mitaa Kata , Tarafa,na Miji.
Amesema kuwa baadhi ya wafugaji
wamekuwa wakiwanyanyasa wakuli kwa kutumia peasa zao hali hii inaleta
manyanyasa na manung’uniko kwa wakulima “ nawaomba sana mkalishughulikie tatizo
hili kwa haraka kwani nyie ndio watendaji wakuu katika maeneo yenu tusisubiri
kamati ya bunge kuja kuchunguza Wakati sisi ndiyo tunaokaa na wananchi”
alisisitiza Mkuu wa Mkoa.
Aidha baadhi ya wajumbe walishauri kuwa maeneo ya serikali, hifadhi za Taifa yasiruhusiwe kuingizwa
kwenye maeneo mapya ya vijiji ili kuondoa migogoro ya wananchi na seikali, hivyo uanzishwaji wa maeneo mapya usiingiliwe na siasa chafu za kuwadanganya wananchi kujichukulia sheria na kuingilia hifadhi za Taifa.
Akihitimisha kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataarifu wajumbe kuwa kikao kijacho cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kutakuwa na shughuli ya kuanza mchakato wa kukusanya fedha za kujenga jengo jipya la Idara ya Wagonjwa wa nje "Out Patients Department" (OPD). zoezi hili lienndana na kufanya harambee kwa wajumbe wote wa kikao.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Luteni Kanali (mst) Issa Salehe Machibya akisisitiza jambo wakati wa kufunga kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kigoma mapema wiki hii. |
No comments:
Post a Comment