Mkuu
wa Mkoa awaomba wananchi kupisha Upanuzi wa Uwanja wa Ndege Mkoani Kigoma
Baada ya kusimama kwa takribani miezi 8 kwa
shughuli za Upanuzi wa Uwanja wa Ndege
Mkoani Kigoma, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya
ameitisha Mkutano na wananchi wa kata za Machinjioni , na Majengo zilizopo eneo
la Manispaa ya Kigoma Ujiji kuwaomba wananchi wapishe upanuzi wa Uwanja wa
Ndege.
Mkutano huu unafuatia wananchi takribani
473 walioathirika na upanuzi wa Uwanja wa Ndege kukataa kuondoka katika maeneo
ya Makazi ambayo Uwanja huo utayafikia baada ya upanuzi. Kufuatia hai hii Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma amelazimika kufanya mazungumzo ya kina na wananchi wa maeneo
haya ili kubaini sababu zinazowafanya wasipishe upanuzi wa Uwanja wa Ndege.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wananchi walisema kuwa wanatambua maendeleo yatakayopatikana baaada ya Uwanja
huo kuruhusu Ndege kubwa kutua, hata hivyo walieleza kuwa hawakupisha eneo hilo
kwani thamani ya malipo ya Tsh 200,000 hadi 300,000 kama fidia ya maeneo ya
Makaburi ya ndugu zao pamoja na Makazi na mali hayakuwa sahihi ukilinganisha na
gharama watakazozipata katika kutafuta viwanja na kujenga katika makazi mapya.
Aidha uthamini wa mali uliofanywa
haukuzingatia muda na mabadiliko ya thamani ya mali na kwamba wananchi
waliotakiwa kuhamishwa hawakuoneshwa viwanja mbadala watakavyoenda kujenga
baada ya kupisha Upanuzi. Hivyo waliiomba serika iweze kuwatazama upya na kuwawezesha
kulingana na thamani ya mali zao ndipo waweze kupisha upanuzi huo.
Mradi wa
ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma kwa kiwango cha rami ambao ulianza
rasmi mwezi Desemba 2011 ukiwa ni mkataba wa miezi (18) uliotegemewa kumalizika
mwezi Juni 2013.
Ukarabati
wa Uwanja wa ndege wa Kigoma unafanyika chini ya Mkandarasi aliyepatiwa kazi
hii Sinohydro Corporation Ltd ya Beijing – China na msimamizi wa Mradi akiwa
Howard Humhureys (Tanzania) Ltd, Steward Scott International (SSI) na
Netherlands Airport Consultant (NACO) ya Netherlands. Maboresho yaliyofanyiwa
kazi hadi Desemba 2012 ni kurefusha njia ya kurukia Ndege kuelekea njia ya
kurukia Ndege Namba 34 kwa mita 450 ikiwemo eneo la tahadhari (Safety zone)
kuelekea njia ya kurukia Ndege namba 16. (Mita 300) na Mfumo wa maji (Drainage
works) kuweka tabaka la kifusi (GS 15) katika umbali wa mita 900 za njia ya
kurukia Ndege. Mradi huu ulitegemewa kuwekea lami eneo la mita 1800, na upana
wa Kiwanja utaongezeka kutoka mita 30 za sasa na kuwa mita 45.
Kumalizika kwa upanuzi wa Uwanja wa
Ndege Mkoai Kigoma utafungua ukurasa mpya kiuchumi kwani nchi za Burundi, Congo
DRC, zitautumia Uwanja huu kama sehemu kubwa ya Usafiri na Usafirishaji. Baada
ya kukamilika kwa upanuzi huu Uwanja wa Ndege wa Mkoani Kigoma utabadilishwa
jina na Kuwa Gombe Mahale International Airport.
Mkuu wa Mkoa amewataka wanchi wawe na
subira kwani Serikali inayafanyia uchambuzi wa kina mawazo yao na kubaini
changamoto juu ya maliop ya fidia za mali zao, hata hivyo aliwaomba wapishe
mradi uendelee huku Serikali ikiendelea kushughulikia matatizo yao na kwamba
waendelee kuiamini Serikali kwani inawathamini wananchi wote.
No comments:
Post a Comment