Thursday, 20 March 2014

Kijiji cha Ilagala chakabidhiwa mradi wenye thamani ya Tsh. 247,556,088.11

         Uongozi unaosimamia Mradi wa Hifadhi ya Ziwa Tanganyika -UNDP/GEF umekabidhi mradi wenye thamani ya Tsh. 247,556,088.11 katika kijiji cha Ilagala Wilayani Uvinza utakaowasaidia wananchi wa eneno hilo katika kukuza kipato kwa uendelezaji wa zao la Mchikichi na pia suala la kutunza Mazingira ya Mto Malagarasi na Ziwa Tanganyika ambapo shughuli hizo zimekuwa zikifanywa na wakazi wa eneo hilo
vitu viliyokabidhiwa ni majengo pamoja na mitambo ya Kisasa ya kuchakatia mazao ya mawese.
Majengo pamoja na Mitambo ya kisasa yaliyokabidhiwa kwa kijiji cha Ilagala.
Mradi wa UNDP/GEF ulikuwa ukijihusisha na utoaji wa elimu ya mazingira, mipango ya matumizi bora ya ardhi, ikiwa pamoja na kuotesha vitalu vya miche ya miti, kutoa mafunzo kwa vitendo juu ya banifu na sanifu kwa ngazi ya jamii na taasisi kama njia mbadala ya kujiongezea kipato.
Fundi sanifu Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bw. Edward Mbuna akielezea mfumo wa maji utakaotumika katika eneo la majengo yaliyokabidhiwa kwa shughuli za kuchakata mafuta ya mawese.
 Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Eng. Dkt. John Ndunguru ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kuitunza miradi hiyo kwa kusimamia sera na sheria ya vyanzo vya maji kwani ndio msingi halisi wa maisha ya mwandamu.
Moja ya sehemu katika Kingo za mto  ambapo shughuli za uchakataji wa Mafuta ya mawese hufanyika kienyeji na kusababisha uchafuzi wa mazingira katika Mto malagarasi na Ziwa Tanganyika.

Hapo awali shughuli za uchataji wa mafuta ya mawese zimekuwa zikifanywa kienyeji na hivyo kusababisha tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira kwani shughuli hizo zilifanyika kwenye kingo za mto Malagarasi unaomwaga maji yake katika ziwa Tanganyika.

Dkt. Ndunguru amawataki vilevile wataalamu wa Kilimo kuanza mchakato wa kuwahamasisha wakulima wa zao la mchikichi kupanda miche mipya ya zao hilo kwani iliyopo sasa imefikia kikomo cha kuendelea kutoa mazao bora
Katibu Wala wa Mkoa wa Kigoma Eng. Dkt. John Ndunguru akikagua matunda ya michikichi ambayo yanaandaliwa kupikwa kienyeji ili kupata mafuta ya mawese.

Katibu Wala wa Mkoa wa Kigoma Eng. Dkt. John Ndunguru akikabidhiwa makabrasha ya mradi kutoka kwa Meneja mradi wa UNDP/GEF Bw. Mushi.

Katibu Wala wa Mkoa wa Kigoma Eng. Dkt. John Ndunguru naye alikabidhi makabrasha ya mradi huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Hadija Nyembo ambapo mradi utawanufaisha wananchi wa Wilaya yake.

Katibu Wala wa Mkoa wa Kigoma Eng. Dkt. John Ndunguru na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Hadija Nyembo wakiwasha mishumaa kama ishara ya kupokea mradi kutoka kwa Meneja wa Mradi wa UNDP/GEF.

No comments:

Post a Comment