Sunday 23 March 2014

Wananchi Waaswa kutunza Miundo mbinu ya maji na vyanzo vya Maji

Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya maji (mwenye suti ya kijivu) Mhandisi Azizi Mutabuzi akiongozana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi Dkt. John Ndunguru kujionea mojawapo ya miradi ya maji katika kijiji cha Nyabitaka Wilayani Kibondo ambako Sherehe za wiki ya Maji zilifanyika Kimkoa.
 Katika kuaadhimisha kilele cha Wiki ya Maji Mkoani Kigoma, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi Dkt. John Ndunguru amewataka wananchi kutunza miundombinu ya maji na vyanzo vya maji ili kuwa na huduma endelevu.

 Katika maadhimisho hayo Katibu Tawala alizindua mradi wa maji uliogharimu zaidi  Shilingi 245 mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya 3000 umefadhiliwa na mashirika mbalimbali zikiwemo nguvu za wananchi na serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzaia.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi Dkt. John Nduguru akivuta maji kwenye Gati la maji lililotengenezwa kwa Msaada wa mashirika ya Concern, TWESA, Bank ya Dunia na Charity Water.



Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Dkt. John Ndunguru akizindua rasmi mradi wa Maji katika kijiji cha Nyabitaka, kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Bw. Leopold Chundu Ulaya, na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Bw. Venance Mwamoto.

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma wakikata Utepe kama Ishara ya kuzindua mradi wa maji ili uanze kutumika rasmi kwa wananchi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Eng. Dkt. John Ndunguru akizindua rasmi huduma ya Maji katika kijiji cha Nyabitaka.

Mmoja wa akinamama akichota maji muda mfupi baada ya mradi wa maji kuzinduliwa rasmi na Katibu Tawala wa Mkoa Eng. Dkt. John Ndunguru.

 Kikundi cha ngaoma aina ya Muyebhe kikitoa burudani siku ya maadhimisho ya wiki ya Maji Mkoani Kigoma.
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Maji Eng. Azizi Muanuzi akiwasilisha kwa Mgeni rasmi Taarifa ya Mkoa kuhusu huduma za Maji Mkoani Kigoma

No comments:

Post a Comment