Wednesday, 5 March 2014

Maafisa Elimu idara ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Kigoma Wakutana kujadili namna ya kuifufua idara hiyo.

 Walimu kutoka katika Idara ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Kigoma wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Afisa Elimu Elimu ya Watu Wazima Mkoa wa Kigoma (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha siku mbili kilichofanyika Mkoani Kigoma kujadili namna ya uboreshwaji wa Elimu ya watu wazima sambamba na kuweka bajeti yenye malengo ya kuinua sekta hiyo.


Afisa Elimu , Elimu ya Watu wazima Mkoa wa Kigoma Bw. Philipo Ntabhiriho akielezea jambo kwa Wakuu wa Idara ya Elimu ya Watu wazima, wakati wa kikao kazi cha maafisa wa Idara hiyo kilichofanyika hivi karibuni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma.


Ukosefu wa Maktaba za kujisomea maeneo ya vijijini unaendelea kuchangia suala la watu kutojua kusoma na kuandika.

Kufuatia hali hii Maafisa Elimu Kitengo cha Elimu ya watu wazima wamekutana Mkoani Kigoma kufanya kikao cha siku mbili kwa lengo la kujenga hoja za Msingi ili waweze kuiomba Serikali kupata fedha za kufufua Elimu ya Watu wazima ambayo inaonekana kuachwa pembeni.

Elimu ya watu wazima inagusa jamii kwa ukaribu kwani watu wakipatiwa elimu nchi itapunguza migogoro mingi inayojitokeza katika jamii mathalani, wakulima, wafugaji  na wafanya biashara.

Moja ya mabo ya Msingi waliyoyawekea kipaumbelea katika mkakati wa kupata fedha ni kupata vitendea kazi na watumishi wa kutosha watakaowezesha kutoa huduma ya Elimu ya Watu wazima.

No comments:

Post a Comment