Wednesday 12 March 2014

Mgogoro kati ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Vijiji vya Mtanga na Mwamgongo Mkoani Kigoma wamalizika.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi  Dkt. John Ndunguru akiwasili kwa Boti ufukweni kwa ziara ya kikazi katika kijiji cha Mtanga kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika.



Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisain katika daftari la wageni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mtanga hivi karibuni, Ziara ambayo iliandaliwa na uongozi wa hifadhi ya ya Taifa ya Gombe kwa lengo la kwenda kutoa taarifa ya kuridhiwa kwa ombi la kurekebisha mpaka wa vijiji vya Mtanga na Mwamgongo vinavyopakana na hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe Dkt. Noelia Muyonga akionesha ramani ya mpaka kati ya kijiji cha Mtanga na Hifadhi ya Gombe ulioridhiwa hivi karibuni

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi Dkt. John Ndunguru akiwa katika msafara wa kukagua alama za mipaka iliyowekwa kutenganisha hifadhi ya Gombe na Kijiji cha mwamgongo kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika.

Baadhi ya viongozi na wanchi wa kijiji cha Mwamgongo wakikagua mpaka mpya kati ya hifadhi ya Gombe na kijiji hicho uliowekwa baada kumalizika kwa mgogoro wa muda mrefu.


Mkuu wa Mkoa akisikiliza maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Kijiji cha Mwamgongo (hayupo pichani) , kushoto kwake ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Gombe Dkt. Noelia Muyonga.


Mgogoro kati ya  Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Vijiji vya Mtanga na Mwamgongo  wamalizika.
Baada ya kudumu kwa takribani miaka 14 hatimaye mgogoro uliokuwepo kati ya Hifadhi ya taifa ya Gombe na Vijiji viwili vya Mtanga na Mwamgongo mwambao wa ziwa Tanganyika umemalizika kwa pande zote mbili kukaa na kuridhia uwekwaji wa mipaka mipya.
Kuisha kwa mgogoro huo kunafuatia uongozi wa hifadhi ya Taifa ya Gombe kufanya jitihada za makusudi kukaa vikao na uongozi pamoja na wanakijiji wa vijiji hivyo ambapo walifikia maridhiano ya  nyumba mbili za makazi kubaki katika eneo la hifadhi na kumegwa kwa eneo la makaburi lililokuwa upande wa hifadhi libaki kwa wananchi.
Aidha kupitia serikali ya Kijiji Hifadhi ya Gombe iliomba kupatiwa eneo la kuelekea ziwani ndani ya maji lenye ukubwa wa kilomita za mraba 21, eneo hilo linataajiwa kuwa eneo maalumu kwa uvuvi wa kitalii na uhifadhi wa mazalia ya Samaki.
Akiongea kwa niaba ya Wananchi Mwenyekiti wa kijiji cha Mtanga Bw. Albert Mrisho alisema anashukuru kuisha kwa mgogoro huu kwani umedumisha uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Vijiji hivyo.

"Hifadhi ya Taifa Gombe inawanufaisha wanakijiji kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kama vile ujenzi wa madarasa, madawati na nyumba za walimu, hivyo kila mwanchi anayaona matunda ya kulinda mahusiano mema ya Hifadhi na kushirikiana nao katika kulinda na kuhifadhi  mazingira" aliongeza mwenyekiti huyo

No comments:

Post a Comment