Mkoa wa Kigoma kuwa
mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya Uchangiaji damu Kitaifa
Mkoa wa
Kigoma utakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu Kitaifa yatakayofanyika
tarehe 14 Juni, 2014 ambapo Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo
atakuwa mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete.
Akitoa
Taarifa ya maadhimisho hayo wakati wa kikao cha hamasa kwa viongozi Katibu
Tawala Msaidizi Seksheni ya Afya Dkt. Leonard Subi aliwaambia wajumbe kuwa
maadhimishohayo yataanza tarehe 1 Juni, 2014 na kumalizika tarehe 14 Juni, 2014
ambayo itakuwa siku ya Kilele.
Dkt. Subi
ameeleza kuwa Halmashauri na Manispaa zitakuwa na vilele vya maadhimisho hayo
kadri ya ratiba itakavyopangwa.
Wananchi
wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika tendo la kuchangia damu ili kusaidia
kuokoa maisha ya kinamama wajawazito na watoto wachanga ambao wengi wao
wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa damu.
Naye
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserkali la Evidence for Action (E4A) Bw.Graig
Ferla alisema vifo vingi vya kinamama
wajawazito vimekuwa vikitokea kabla au mara baada ya kujifungua, suala la
ukosefu wa damu katika hospitali limekuwa ni kubwa.
Alitoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa
kuchangia damu kwa hiari na kuliweka suala hili kama agenda ya kila mara katika
jamii ili kunusuru vifo vya kinamama na watoto.
Katibu Tawala Seksheni ya Afya, Dkt.
Leonard Subi akitoa takwimu za vifo vya
kinamama na watoto wachanga za kila
Wilaya Mkoani Kigoma ambapo Mkoa umejitahidi kupungua vifo hivyo kwa kiwango
kikubwa.
|
Habari na Picha- G.D. Ng'honoli (Afisa Habari wa RS)
No comments:
Post a Comment