Monday 28 April 2014

NMB kuchangia vifaa Tiba vyenye tahamni ya Tshs 10,000,000 katika Hospitali ya maweni Mkoani Kigoma



NMB kuchangia vifaa Tiba katika Hospitali ya maweni
Benki ya Taifa ya Biashara NMB imesema itachangia vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni kumi (10,000,000) katika Hospitali ya Rufaa ya Maweni Mkoani Kigoma.


Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tawi la Benki hiyo Meneja wa Kanda wa Benki ya NMB Bw. Ibrahim Agustino alisema kwa kutambua mchango mkubwa na ushirikiano wa wateja na ungozi wa Mkoa wa Kigoma Benki ya NMB imeona ni muhimu kuchangia huduma za Afya ili wananchi waendelee kuwa na afya njema nahivyo kuendelea na Shughuli za uzalishaji mali na kukuza kipato.


Naye Meneja wa tawi la Benki ya NMB Mkoa wa Kigoma Bw. Rodgers Malangu alisema tendo la NMB kuchangia katika afya ni moja ya malengo yake katika kujenga mahusiano mazuri kati ya wateja, jamii na Serikali kwa ujumla.
 Alisema kwa sasa Benki hiyo inatarajia Kufungua matawi yake sehemu zote za Wilaya mpya hususan Buhigwe, Uvinza na Kakonko.

Bw. Rodgers Malangu ambaye ni Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Mkoani Kigoma akitoa maneno ya Ukaribisho wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa Tawi la Benki hiyo Mkoani Kigoma


Meneja wa Kanda wa Benki ya NMB Bw. Ibrahim Agustino akitoa hotuba wakati wa Uzinduzi wa Tawi la Benki ya NMB Mkoani Kigoma.


Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Ramadhan Maneno akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Tawi la Benki ya NBM kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa (mgeni rasmi).



Mkuu wa Wilaya ya Kigoma , Mhe. Ramadhan Maneno akiondoa kitambaa katika jiwe la Msingi la NBM kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma; kushoto kwake ni Meneja wa Kanda wa Benki hiyo Bw. Ibrahim Agustino, na wa mwisho kushoto ni Meneja wa Tawi Mkoani Kigoma Bw. Rodgers Malangu.


Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Ramadhan Maneno (katikati) akikata Utepe kama ishara ya Kuzindua tawi la NMB Mkoani Kigoma, kulia kwake ni Meneja wa Kanda wa Benki hiyo Bw. Ibrahim Agustino, na kushoto ni Meneja wa Tawi Mkoani Kigoma Bw. Rodgers Malangu.


Meneja wa NMB tawi la Kigoma Bw. Rodgers Malangu akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Mhe. Ramadhan Maneno  namna Benki ya NMB inavyowahudumia wateja wenye mahitaji mbalimbali ya kibenki.


Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mhe. Gishuli Charles akipata huduma katika moja ya kaunta zilizopo NMB Tawi jipya la Kigoma mara baada ya kuzinduliwa. Aliyesimama kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Ramadhani Maneno.



No comments:

Post a Comment