Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.
Brigedia Generali (Mst.) Emannuel Maganga leo ameongoza na kushiriki mazoezi ya
mbio kwa umbali wa kilomita 12 zilizolenga kuhamasisha watu wapende kufanya
mazoezi ya mwili ili kuimarisha Afya zao.
Mbio hizo zilizoandaliwa na Kigoma Jogging Club zimehudhuriwa na
viongozi mbalimbali wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, watumishi
kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Taasisi
mbalimbali za Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Katika kuhitimisha mbio hizo
Brigedia Generali (Mst.) Maganga amewashukuru Uongozi wa Kigoma Jogging Club
kwa kuanzisha mazoezi hayo ambayo ni muhim kwa afya “ nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza ninyi mliofikiri
kuanzisha kitu kama hiki kwani leo tulivyokimbia pamoja tumepata faida nyingi,
ukiachiliambali kujenga afya tumefahamiana na kujenga umoja, hata hivyo baadhi
yetu hufanya mazoezi haya kwa ratiba zao lakini tunapokuwa pamoja hivi
tunatiana moyo zaidi kuliko mtu akifanya mazoezi peke yake anaweza kujisikia
uvivu na kuacha”
Aidha amewaasa watumishi
wote na wananchi kupenda kufanya mazoezi kama njia ya kuondokana na maradhi
mbalimali mathalani shinikizo la damu. “Ninawaomba msiishie leo tu, mazoezi
haya yawe endelevu kwa ajili ya faida ya afya zetu”
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia
Generali (Mst.) Emannuel Maganga akiwa na Wakuu wa Taasisi, Idara mbalimbali
wakati wa kukimbia mbio za uhamasishaji Mazoezi
|
Watumishi kutoka sekta mbalimbali katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wakishiriki mbio za uhamasishaji wa Mazoezi kama sehemu ya kuboresha Afya zao. |
No comments:
Post a Comment